MWANAUME AJINYONGA KISA WIVU WA MAPENZI

MCHIMBA migodi mmoja huko Migori, Kenya, amejinyonga baada ya mkewe kudai kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine.
Mtu huyo, James Juma (30) alijinyonga jana usiku baada ya kugundua kwamba mkewe na watoto wake walikuwa wameondoka na kumwacha peke yake.
“Alipofahamu mke wake kamuacha, aliingia katika nyumba aliyopanga na kutumia kamba kujinyonga,” alisema Samuel Yogo, kiongozi wa kitongoji cha Suna-Chini na kuongeza kwamba majirani waliingiwa na wasiwasi walipoona ukimya kwenye nyumba ya Juma baada ya kupita saa nne asubuhi.
“Walipochunguza, walimkuta amekufa chumbani mwake,” alisema Yogo ambapo ndugu waliuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka Hospitali ya Rufaa ya Migori wakati upelelezi wa polisi ukiendelea
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post