MWANZA: MTOTO ALIWA NA FISI AKISUBIRI CHAKULA CHA USIKU

SHARE:

Tarehe 24.07.2017 majira ya saa 11:00 alfajiri katika Mtaa wa Kabangaja Kata ya Bugogwa Wilaya ya Ilemela jiji na Mkoa wa Mwanza, makusud...

Tarehe 24.07.2017 majira ya saa 11:00 alfajiri katika Mtaa wa Kabangaja Kata ya Bugogwa Wilaya ya Ilemela jiji na Mkoa wa Mwanza, makusudi Rashidi miaka 39, mkazi wa Mtaa wa Ibangaja, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 11 (jina tunalihifadhi) na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri, kitendo ambacho ni kosa la jinai.
Awali inadaiwa kuwa, alfajiri ya majira tajwa hapo juu wazazi wa majeruhi aliyebakwa waliondoka na kwenda kutafuta riziki ya watoto huku nyumbani wakiwaacha majeruhi na mdogo wake wakiwa wamelala. Inasemekana kuwa wakati majeruhi akiwa amelala na mdogo wake, ghafla alishtuka na kumuona mtuhumiwa tajwa hapo juu akiwa anambaka kwa nguvu huku akisikia maumivu makali na kupelekea kupiga kelele za yowe akiomba msaada, inadaiwa kuwa baada ya mtuhumiwa kuona hali hiyo alitoka nje na kuanza kukimbia.
Wananchi walifika kwa haraka eneo la tukio kutoa msaada ambapo baada ya kufika walimuona mtuhumiwa akiwa anakimbia na kuanza kukimbiza hadi walifanikiwa kumkamata kisha wakatoa taarifa kituo cha polisi, askari walifanya ufuatiliaji wa haraka juu ya taarifa hizo hadi eneo la tukio na kumkuta mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi wa wananchi.
Polisi wapo katika mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani, majeruhi tayari amepelekwa hospitali kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishina wa Polisi, Ahmed Msangi ametoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa wa mwanza hususani wazazi/walezi akiwaomba kuwa na makazi salama yatakayoweza kuwalinda watoto na mali dhidi ya wahalifu. Aidha pia amewataka wananchi wa Mwanza kuwa waangalifu na makini wakati wote na watu wenye nia ovu dhidi ya watoto.
Katika tukio la pili;
Mnamo tarehe 23.07.2017 majira ya 9:00 jioni katika Kitongoji cha Izizimba, Kijiji cha Izizimba “A” Kata ya Mhande, Tarafa ya Mwamashimba, Wilaya ya Kwimba, Mkoa wa Mwanza, mtoto wa kike aliyefahamika kwa jina la Limi Bunzama, miaka 04, mkazi wa Kijiji cha Izizimba “A”, amefariki dunia baada ya kukamatwa na fisi wakati akiwa anacheza na baadae kuliwa sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kufariki dunia.
Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa na mama yake nje ya nyumba yao akiwa anacheza huku wakiwa wanasubiri chakula cha usiku. Inasemekana kuwa wakati marehemu akiwa anacheza mbali kigodo na alipo mama yake ghafla alifika mnyama fisi na kumkamata kisha kukimbia nae vichakani. Mama wa marehemu alisikia kelele za mtoto wake akilia ndipo alianza kumfuatilia huku akipiga yowe akiomba msaada.
Inasemekana kuwa majirani walifika eneo la tukio na kushirikiana na wazazi wa marehemu kumfuatilia fisi huyo, lakini kwa bahati mbaya walichelewa kwani walikuta  tayari fisi amemuua mtoto na kumla sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kukimbia kichakani. Aidha mabaki ya mwili wa marehemu tayari yamefanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi. Chanzo cha kifo hicho ni uzembe wa wazazi kutokuwa makini na motto.
Juhudi za kumtafuta fisi huyo ili asiendelee kuleta madhara kwa watu na watoto kwa kushirikiana na wananchi bado zinaendelea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishina wa Polisi, Ahmed Msangi ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza hususani wazazi na walezi akiwataka kuwa waangalifu na makini wakati wote na watoto, ili kuwaepusha na ajali au na vifo vinavyoweza kuepukika.
Imetolewa na:
DCP: Ahmed Msangi
Kamanda wa Polisi (M) Mwanza

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MWANZA: MTOTO ALIWA NA FISI AKISUBIRI CHAKULA CHA USIKU
MWANZA: MTOTO ALIWA NA FISI AKISUBIRI CHAKULA CHA USIKU
https://2.bp.blogspot.com/-7rKQ7iqXbEw/WXhWZxEt7PI/AAAAAAAAdEY/683AOF1eqX4b8yccKZbhcA1DVrLZJNMBQCLcBGAs/s1600/xCrocuta_crocuta_Mara_Triangle-750x375.jpg.pagespeed.ic.0LRImW6WUw.webp
https://2.bp.blogspot.com/-7rKQ7iqXbEw/WXhWZxEt7PI/AAAAAAAAdEY/683AOF1eqX4b8yccKZbhcA1DVrLZJNMBQCLcBGAs/s72-c/xCrocuta_crocuta_Mara_Triangle-750x375.jpg.pagespeed.ic.0LRImW6WUw.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/07/mwanza-mtoto-aliwa-na-fisi-akisubiri.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/07/mwanza-mtoto-aliwa-na-fisi-akisubiri.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy