MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI TFF AIKIMBIA DAR, ATUA MWANZA

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Revocatus Kuuli ambaye kamati yake ilikuwa gumzo hivi karibuni kutokana na mchakato wa uchaguzi unaendelea kwenye Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) amesema ameamua kuondoka ndani ya Dar es Salaam.
Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa na msimamo tofauti na wajumbe wenzake juu ya kilichokuwa kikiendelea baada ya usaili wa wagombea wa uchaguzi huo, wiki iliyopita amesema aliamua kuondoka Dar na kwenda Mwanza kwenye shughuli zake binafsi.
Kuuli amesema hayo jana jioni alipoulizwa juu ya kinachondelea baada ya kamati hiyo kuvunjwa na kisha kuundwa upya ambapo jina lake ndilo pekee lililobaki katika kamati mpya huku wajumbe wengine wote wakibadilishwa.
Amesisitiza kuwa yupo Mwanza lakini akipata barua ya kuitwa Dar atageuka haraka kwa kuwa hakuna umbali mkubwa kati ya majiji hayo mawili.

Tujikumbushe wajumbe walioondolewa katika kamati ya uchaguzi ni: 
1. Juma Lalika
2. Dominated Madeli
3. Jeremiah Wambura
4. Omary Hamidu

Wajumbe wapya wa kamati hiyo chini ya Wakili Revocatus Kuuli ni:
1. Mohammed Mchengela
2. Wakili Malangwe Ally
3. Wakili Kilomoni Kabamba
4. Wakili Deus Kalua
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post