NAFASI YA JAMAL MALINZI TFF YAPATA MRITHI

Siku chache baada ya kuswekwa rumande kwa tuhuma za makosa ya matumizi mabaya ya ofisi, Rais wa Shrikisho la Soka Tanzania (TFF) pamoja na makamu wake wamepata warithi wakushikilia nafasi zao.
Kamati ya utendaji ya TFF iliyokutana leo Jumamosi asubuhi kwa dharua imeteau viongozi wawili kukaimu nafasi hiyo ya viongozi wa juu wa TFF ambao wamepelekwa rumande kufuatia mashtaka 28 waliyosomewa mapema wiki hii.
Walioteuliwa kushika nyadhifa hizo ni, Makamu wa Rais, Wallace Karia ambaye ameteuliwa kukaimu nafasi ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi huku Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi akiteuliwa kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Selestine Mwesigwa ambaye naye yuko rumande.
Jamali Malinzi na Selestine Mwesigwa wapo rumande tangu Alhamisi Juni 27 mwaka huu baada ya kukosa dhamana na wanatarajiwa kurudishwa tena mahakamani Jumatatu Julai 3 mwaka huu.
Kamati hiyo imesema kuwa imelazimika kukutana kwa dharura ili kuhakikisha kuwa shughuli za TFF zinakwenda sawa licha ya viongozi hao kutokuwapo, kwani moja ya shughuli kubwa ni maandalizi ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Salum Madadi alisema, kwa mujibu wa katiba ya TFF kifungu cha 35 (I) na 35 (6) imeeleza ulazima wa kuitishwa kikao cha kamati ya utendaji ili kutengeneza utaratibu wa shughuli za shirikisho kuendelea.
Aidha alisema kuwa shughuli za kukamimu nafasi hizo zitaendelea hadi pale viongozi hao watapobainika kuwa hawana hatia (mwisho wa mashtaka).
Malinzi ambaye alikuwa miongoni mwa wagombea wa kiti cha urais wa TFF, atashindwa kutetea nafasi hiyo aliyoitumikia kwa miaka minne kwa sababu hajatokeza kwenye usaili wa wagombea ambao umefikia tamati leo kutokana na kushikiliwa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post