NDUGU WA WALIOFARIKI KWENYE MGODI WA ACACIA WAISHTAKI KAMPUNI HIYO UINGEREZA

Kampuni inayomiliki migodi mitatu inayoendesha shughuli za uchimbaji madini nchini, Acacia imefunguliwa kesi nchini Uingereza na ndugu wa watu waliofariki katika moja ya migodi yao. Kampuni hiyo ambayo kwa sasa imo kwenye mgogoro mkubwa na Serikali ya Tanzania kuhusu malimbikizo ya kodi ambazo hazijalipwa inaweza kuhitajika kulipa fidia watu hao wanaowakilishwa na mawakili kutoka katika kampuni inayotoa msaada wa kisheria nchini Uingereza, Deighton Pierce Glynn.
Mawakili hawa wamefungua kesi 10 ambazo nyingi kati ya hizo ni kutokana na matukio yaliyotokea mwaka tangu mwaka 2013 na moja ni tukio la mwaka jana 2016 katika mgodi wa Noth Mara unaomilikiwa na kampuni hiyo, ikiwa ni mmoja kati ya migodi mitatu inayoimiliki hapa nchini.
Inaeleweka kwamba mawakili hao wanashughulika na madai yaliyopo kwamba kampuni ya Acacia haitoi fidia iliyotakiwa kwa ndugu wa watu waliofariki kwenye mgodi huo. North Mara umekuwa ni mgodi ambao kwa mianga mingi sasa umekuwa ukikumbwa na matukio ya watu kuingia bila idhini na kuchimba madini bila utaratibu na kwamba watu wengi wamekuwa wakiuawa ndani ya mgodi kutokana na matukio ya aina hiyo.
Serikali ya Tanzania iliripoti mwaka jana kuwa kuanzia mwaka 2006, madai ya vifo ya watu 65 waliouliwa na polisi na walinzi ndani ya eneo la mgodi wa North Mara yaliripotiwa na kwamba majeruhi wanasemekana kuwa zaidi ya 270.
Kampuni ya Acacia imepinga idadi hii lakini ikakubali kwenye ripoti yake ya mwaka iliyotoka mwanzoni mwa mwaka huu kwamba kulikuwa na matukio ya uvamizi sita mwaka 2016 katika mgodi huo, ambapo mawili kati ya hayo “yalihusishwa uwepo wa polisi kuyatatua.”
Pia, ripoti hiyo imesema kulikuwa na vifo tisa mwaka 2015 na vifo 17 mwaka 2014 lakini Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Brad Gordon ameliambia gazeti la Daily Telegraph kwamba hali hiyo “imeimarika sana” katika kipindi cha miaka minne iliyopita ikiwa ni matokeo ya mafunzo na uzio uliowekwa kwenye migodi yao, na kuongeza kuwa kampuni hiyo “inajivunia” kwa kazi kubwa iliyofanya kuimarisha uhusiano na wananchi.
Ikijibu maandamano yaliyofanywa na kundi la watetezi wa haki za binadamu mwanzoni mwa mwezi huu, Acacia imesema kwamba kampuni hiyo imekuwa moja ya kampuni chache kuchapisha habari za matukio ya vifo kwa watu ambao si wafanyakazi wa mgodi huo.
Imesema kuwa “tutahakikisha tunafata njia sahihi kabisa kuipinga… na tutalishughulikua kwa njia sahihi.” Mwaka 2015, Acacia ilifikia makubaliano ya nje ya mahakama na watu tisa waliofungua kesi ya madai nchini Uingereza kuhusiana na vifo vilivyotokea katika mgodi wa North Mara vilivyotokea kabla ya mwaka 2013, kipindi hicho ikiwa inaitwa African Barrick Gold.
Mgodi wa North Mara ulihusisha mapigano ya silaha mwezi uliopita pale wanakijiji waishio karibu walipovamia mgodi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post