NESI MKOANI GEITA ADAIWA FIDIA YA MIL. 200 KWA KUTOA LUGHA CHAFU

Uongozi wa Hospitali binafsi ya Makoye mkoani Geita kupitia kwa kampuni ya uwakili ya Rock ya jijini Mwanza imetoa notisi ya siku 14 kwa Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, Mary Muntu kulipa fidia ya shilingi milioni 200 kwa madai ya kutumia lugha ya kashfa kwa watumishi wa Makoye.
Chanzo cha madai hayo, hati inasema, ni lugha iliyotumiwa na Muntu kwa baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Makoye waliokwenda Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Geita Juni 1 kumjulia hali mteja wao.
Imedaiwa katika hati hiyo kuwa siku hiyo asubuhi, Muntu akiwa Muuguzi kiongozi wa zamu hospitalini hapo anadaiwa kuwaambia watumishi wa hospitali ya Makoye kuwa hawana shule.
Akizungumzia hatua hiyo, Renatus Mnaku (Ofisa Masoko na Mahusiano wa hospitali ya Makoye) alisema alishambuliwa kwa maneno na muuguzi huyo walipokwenda hapo kwa lengo la kumjulia hali mteja wao.
Mnaku alisema kuwa muuguzi huyo alitoa maneno hayo mbele ya watu katika eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na kwamba aliendelea licha ya kwamba alimsihi kuwa yalikuwa yanaivunjia hadhi Hospitali ya Makoye kwa kudai kuwa watumishi wake hawakusoma.
Muntu alikiri kutokea majibizano kati yake na watumishi wa Makoye alipokuwa msimamizi wa zamu lakini akadai hakumbuki kama alitoa maneno ya kashfa kama inavyodaiwa. Muntu alisema kuwa amepokea notisi ya madai kutoka kampuni ya mawakili ya Rock ikimtaka kulipa fidia ya shilingi milioni 200, lakini yeye hana uwezo wa kulipa fedha hizo.
Alisema kuwa serikali ndiyo itakayopaswa kuwajibika kwa hilo kwa sababu siku ya tukio alikuwa yupo kazini. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita, Dkt. Joseph Kisala alisema kuwa malalamiko juu ya matumizi ya lugha chafu kwa wagonjwa na ndugu zao yalikuwa yakijitokeza katika siku za nyuma lakini vitendo hivyo vilikoma baada ya kuvikemea.
Aidha, Dkt. Kisala alisema kuwa ana taarifa ya kutokea kutoelewana kati ya Muntu alipokuwa zamu kama muuguzi msimamizi siku hiyo na watumishi wa Makoye, lakini akaahidi kufatilia ili kufanyia kazi sintofahamu hiyo. Alimshauri kuwa ingekuwa vizuri tatizo hilo likamalizwa kwa kupatikana suluhu.
HT @ NIPASHE
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post