NHC YAAGIZWA KUJENGA NYUMA KATIKA MAENEO YOTE MAPYA YA UTAWALA

SHARE:

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la nyumba Nchini kwenda kujenga nyumba bora za makazi katika maeneo yote mapya ya utawala ...

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la nyumba Nchini kwenda kujenga nyumba bora za makazi katika maeneo yote mapya ya utawala ikiwemo mikoa na wilaya ili kusaidia kutatua changamoto ya makazi kwa watumishi.
Pia ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe zinazojengwa katika kijiji cha Tindingoma, unaojengwa na Shirika la Nyumba Nchini.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Julai 21, 2017) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Naming’ongo wilaya ya Momba akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Songwe.
“Nalipongeza Shirika la Nyumba kwa mikakati waliyonayo ndani ya shirika hilo na kwamba waendelee na utekelezaji wa mipango hiyo ya ujenzi wa nyumba ili maeneo yote mapya ya utawala yaweze kuwa na makazi bora ya kuishi watumishi.”
Pia aliwataka wakazi wa kata ya Chitete yaliko makao makuu ya wilaya ya Momba kuhakikisha wanachangamkia fursa ya uwepo wa makao makuu wa wilaya kwenye kata yao kwa kujenga nyumba za kisasa kwa ajili ya kupangisha watumishi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Nehemia Mchechu amesema mradi huo wenye thamani ya sh bilioni 2.2 ulianza kujengwa Machi 2016 na unatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu.
Amesema mradi huo ulibuniwa baada kupokea maombi kutoka Halmashauri ya wilaya ya Momba na kwamba unatekelezwa kwa awamu mbili ya kwanza ni ujenzi nyumba nane na tayari zimekamilika.
Ameongeza kwamba ujenzi wa awamu ya pili unajumuisha nyumba tisa ambapo gharama ya ujenzi wa nyumba itatumika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya ofisi za Halmashauri hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya NHC , Bi. Blandina Nyoni amesema shirika hilo lilianzisha mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwawezesha wananchi kuwa na makazi bora.
Amesema katika miradi 54 ya ujenzi wa nyumba inayotekelezwa na shirika hilo katika maeneo mbalimbali nchini kati yake miradi 24 imekamilika ikiwemo 14 ya nyumba za gharama nafuu.
Pia Mbunge wa jimbo la Momba (CHADEMA), David Silinde amesema anashukuru Serikali kwa ujenzi wa nyumba hizo na kumueleza Waziri Mkuu kwamba wananchi wa Momba wanaridhishwa na utendaji wa Serikali na kwamba maendeleo hayana chama.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JULAI 21, 2017

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: NHC YAAGIZWA KUJENGA NYUMA KATIKA MAENEO YOTE MAPYA YA UTAWALA
NHC YAAGIZWA KUJENGA NYUMA KATIKA MAENEO YOTE MAPYA YA UTAWALA
https://4.bp.blogspot.com/-jcgK9MK736k/WXL-2yfuFzI/AAAAAAAAc6s/uUxo-1bpAOcTIyxXaa5AWQsxcl9_u9mugCLcBGAs/s1600/xDSC7351-750x375.jpg.pagespeed.ic.w7f1agnyBC.webp
https://4.bp.blogspot.com/-jcgK9MK736k/WXL-2yfuFzI/AAAAAAAAc6s/uUxo-1bpAOcTIyxXaa5AWQsxcl9_u9mugCLcBGAs/s72-c/xDSC7351-750x375.jpg.pagespeed.ic.w7f1agnyBC.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/07/nhc-yaagizwa-kujenga-nyuma-katika.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/07/nhc-yaagizwa-kujenga-nyuma-katika.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy