NIYONZIMA AULIZWA ‘UTACHEZA SIMBA AU YANGA?’ AMEJIBU HIVI...

Kiungo Haruna Niyonzima amezungumza kwa mara ya kwanza juu ya taarifa za usajili wake baada ya kuelezwa kuwa kila kitu tayari na atatua Simba siku si nyingi.

Akizungumza baada ya mchezo wa Rwanda dhidi ya Taifa Stars uliochezwa juzi Jumamosi jijini Kigali nchini Rwanda, akiwa ni mmoja wa watazamani, Niyonzima aliulizwa juu ya mwelekeo wake wakati akiuchambua mchezo baina ya timu hizo mbili uliomalizika kwa suluhu.

“Ulikuwa mchezo mzuri na watazamaji wamepata burudani nzuri,” alisema Niyonzima, alipoulizwa kuhusu mwelekeo wake katika msimu ujao, mchezaji huyo anayesifika kwa kachumbari za uwanjani, alisema:

“Mambo yangu siyafanyi wazi, nayapeleka mambo kimyakimya, kuhusu wapi nitacheza muda utafika na nitaweka wazi, siwezi kulizungumzia hilo kwa sasa.”
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post