NJIA RAHISI YAKUONDOKA MICHIRIZI KWENYE NGOZI KWA KUTUMIA LIMAO NA SUKARI

Michirizi inayotokana na kuongezeka kwa uzito huwa haivutii katika ngozi. Lakini hili linaweza lisiwe kwa watu wote kwani baadhi ya wanaume hupenda kuona michirizi hiyo kwenye miili ya wapenzi wao.
Michirizi hiyo ambayo mara nyingi hutokea tumboni, kwenye mapaja, kwenye mikono na kiunoni, baadhi ya watu huiona kama ni doa katika ngozi zao na hivyo kutamani kuiondoa.
Zipo njia za asili za kuzuia michirizi, lakini pia zipo njia za kutibu ingawa huchukua muda mrefu kutoa matokeo hivyo huhitaji uvumilivu.
Moja ya njia za asili ni matumizi ya juisi ya limao iliyochangaywa na sukari nyeupe na mafuta ya almond.
Jinsi ya kuandaa.
Kamua limao moja kila siku na uchanganye na kijiko cha sukari nyeupe na mafuta ya almond.
Paka mchanganyiko huo katika eneo lililoathirika kisha sugua taratibu kwa muda wa dakika tatu. Kabla ya kuosha au kuoga, acha kwanza mchanganyiko huo ukae juu ya ngozi kwa dakika moja.
Jikaushe na kisha paka mafuta au losheni ambayo haina kemikali za mercury na hydroquinone .
Fanya hivi kwa muda wa wiki saba utaona michirizi ikipotea taratibu.
-MWANANCHI
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post