NJIA WANAZOTUMIA MABILIONEA KUBANA MATUMIZI ILI WAFANIKIWE ZAIDI

SHARE:

Ubahili ni neo lenye maana tofauti kwa watu tofauti. Kwa mwingine kitendo cha kula nyumbani au kutafuta hoteli na maduka yenye bidhaa zil...

Ubahili ni neo lenye maana tofauti kwa watu tofauti. Kwa mwingine kitendo cha kula nyumbani au kutafuta hoteli na maduka yenye bidhaa zilizo kwenye punguzo la bei kwake ni ubahili.
Lakini kwa mtu ambaye ni bilionea yaweza ikawa ni kuja kazini akiwa amevaa fulana na jizi, kuendesha gari ya bei rahisi, na wakati mwingine ni kwa kununua ndege binafsi au jumba la kifahari kwa gharama nafuu.
Cha ajabu ni kwamba baadhi ya watu matajiri zaidi ulimwenguni ni mabahili kupita kiasi, kila mmoja akiwa na njia zake binafsi za kubania pesa zake.
Wengine wanabania matumizi kwa kula chakula cha ofisini pamoja na wafanyakazi na wengine kuishi kwenye nyumba za gharama ndogo kulinganisha na utajiri wao, mabilionea hawa nane — ambao wengi wao wanatoa sana misaada — wanajua njia za kutunza utajiri wao ili waendelee kubaki juu.

Warren Buffett, bado anaishi kwenye nyumba aliyonunua mwaka 1958.

Kiwango cha utajiri: Dola bilioni 74 (trilioni 165.7)
Bilionea huyu wa jijini Omaha ni mmoja kati ya mabilionea wenye busara na bahili zaidi walio hai kwa sasa. Ingawa ni mmoja kati ya watu matajiri zaidi ulimwenguni, mpaka sasa bado anaishi kwenye nyumba yake ya kawaida aliyoinunua mwaka 1958, kipindi hicho alinunua kwa shilingi milioni 70 za kitanzanua, hana simu ya mkononi wala kompyuta kwenye ofisi yake na kuna kipindi aliwahi kutengeneza kibao cha gari yake kilichoandikwa “THRIFTY (ikimaanisha mtu mwenye tabia ya kutumia kwa uangalifu wa hali ya juu pesa zake na vitu vyake vingine) – kwa mujibu wa wasifu wake uliochapishwa mwaka 2009. N rafiki yake mkubwa kwa miaka 25 sasa, Bill Gates anapotembelea jijini Omaha, Buffett huenda yeye mwenyewe uwanja wa ndege kumpokea Gates.
Katika mkutano wake na wawekezaji wa kampuni zake uliofanyika mwaka 2014, Buffett alieza kwamba kiwango chake cha maisha hakiathiriwi na kiasi cha pesa alichonacho:
“Maisha yangu hayawezi kuwa mazuri na yenye furaha zaidi ya niliyonayo sasa. Yangekuwa mabaya zaidi kama ningekuwa na nyumba sita au nane. Kwahiyo, nina kila kitu ninachotakiwa kuwa nacho na sihitaji kitu kingine chochote kwa sababu inafika mahali wingi au uchache wa vitu unavyomiliki hauleti tofauti yoyote maishani.”

Mark Zuckerberg, muanzilishi wa Facebook, bado anaendesha gari yake aina ya Volkswagen.

Kiasi cha utajiri: dola bilioni 70 (trilioni 156.7)
Ingawa anajulikana kama miongoni mwa matajiri wakubwa zaidi duniani kutokana na nyanja ya teknolojia, Mark Zuckerberg anaishi maisha ya hali ya kawaida sana pamoja na mkewe Priscilla Chan na mtoto wao. Muanzilishi huyu wa mtandao wa kijamii wa Facebook amekuwa hana aibu kuonekana akivaa fulana ya kawaida na jinzi tu ingawa ana pesa za kuweza kununua nguo ghali zaidi kutoka kwa wabunifu maarufu wa mitindo duniani.
“Kwakweli nataka kuwa na maisha ya kawaida kabisa ili nibaki na mambo machache sana ya kuyatolea maamuzi kuhusu jambo lolote isipokuwa kufikiria jinsi gani ya kuwafikia watu wengi kirahisi zaidi,” alisema Zuckerberg.
Vishawishi vinavyoambatana na utajiri havijawahi kumtisha bilionea huyu mwenye miaka 33 kwani mwezi Disemba, 2015 alitangaza kwamba katika maisha yake, asilimia 99 ya hisa zake za Facebook atazitoa kusaidia maswala mbalimbali duniani.

Amancio Ortega, anakula chakula cha mchana na wafanyakazi wake mpaka sasa

Kiasi cha utajiri: dola bilioni $82.3 (trilioni 184.3)
Biilionea huyu pia aliwahi kusema kuwa kiasi cha pesa alichonacho hakiathiri jinsi ya kuendesha maisha yake. Ortega amekuwa akiishi maisha ya kutojulikana kabisa kwa muda mrefuwa maisha yake, na akiwa likizo huenda kwenye nyumba yake iliyopo nchini Uhispania pamoja na mkewe, hununua kahawa yake kwenye mgahawa mmoja tu siku zote, na kula chakula cha mchana na wafanyakazi wake kila siku ya kazi.
Kama bilionea mwenzake wa Facebook, Ortega huwa anavaa sare yake ya kawaida kabisa. Koti la suti la rangi ya bluu, shati jeupe na suruali ya kijivu ambayo huivaa kila siku. Baadhi ya watu wanasema kuwa hastahili kuitwa bahili kwakuwa anamiliki ndege binafsi aina ya Bombardier aliyoinunua kwa zaidi ya bilioni 100, lakini huwa hasafiri sana kwakuwa muda mwingi huwa anakuwa kazini.

Carlos Slim HelĂș, ameishi kwenye nyumba yake kwa zaidi ya miaka 40 sasa

Kiasi cha utajiri: dola bilioni 65.3 (trilioni 146.2)
Badala ya kutumia utajiri wake unaopanda na kushuka, Carlos Slim anawekeza mabilioni yake kwenye kukuza uchumi na kampuni zake nyingi. Kuna kipindi aliwashangaza waandishi wa Reuters alipowapa mfano kwamba utajiri ni sawa na bustani kwa sababu “unachotakiwa ni kuhakikisha ulichokipanda kinakuwa, endelea kuwekeza zaidi kwenye biashara hiyohiyo ili kukifanya kikue zaidi au wekeza kwenye biashara nyingine.”
Bilionea huyu mwenye miaka 77ndio tajiri namba moja nchini Mexico lakini hapendi anasa kama ndege au boti binafsi za kifahari na imeripotiwa kuwa mpaka sasa bado anaendesha gari yake toleo la zamani aina ya Mercedes-Benz. Slim anaendesha makampuni yake kwa ubahili wa hali ya juu sana pia, akiwaasa wafanyakazi wake kwamba muda wote wahakikishe “wasifanye matumizi mabaya kisa wanaona mambo yanawaendea vizuri (wakati ambao ng’ombe amenawiri vizuri na anatoa maziwa mengi).”
Mfanyabiashara huyu ameishi kwenye nyumba yake ya vyumba sita nchini Mexico kwa zaidi ya miaka 40 na mara nyingi anakula nyumbani na wanae pamoja na wajukuu. Ana vitu anavyovipenda na vinavyojulikana ikiwamo kuchora — ikiwa ni kumbukumbu kwa marehemu mke wake — na kuvuta sigara zinazotengenezwa nchini Cuban.

Ingvar Kamprad, bado anasafiri daraja la kati kwenye ndege na anapanda basi mpaka sasa

Kiasi cha utajiri: dola bilioni $43.8 (trilioni 98)
Kamprad ni miongoni mwa watu matajiri zaidi barani Ulayalakini hutajua endapo utakaa pembeni yake mkiwa mnasafiri pamoja kwenye ndege kwenye daraja la kati au mkiwa mnakula kwenye mgahawa. Mara ya mwisho aliyowahi kutumia pesa nyingi ni miaka ya 60 aliponunua gari aina ya Porsche na kuvaa nguo zilizoshonwa na wabunifu wa mavazi, Bilionea huyu wa nchini Sweden ambaye anafanya biashara ya samani amekuwa na sifa ya kuwa bahili sana — wengine wanamuita mtu anayependa vitu vya bei rahisi — ingawa ana mabilioni ya pesa, ikiwemo kuendesha gari lake aina ya Volvo alilokaa nalo kwa zaidi ya miaka 20 na kupanda usafiri wa mabasi.
Tajiri huyu mwenye umri wa miaka 91 anamiliki zaidi ya trilioni 98, lakini alihamia nchini Sweden mwaka 2013 baada ya kuishi nchini Uswisi kwa miaka 40 — alipokuwa akikwepa kodi kubwa za nchini Sweden.

Charlie Ergen, bado anabeba chakula toka nyumbani ili akale kazini

Kiasi cha utajiri: dola bilioni: 19.9 (trilioni 44.5)
Charlie Ergen ni mfanyabiashara anayesifika kwa kuwa bahili kupita kiasi, lakini pia anaendeleza tabia hii hata kwenye maisha yake binafsi. Bilionea huyu mwenye umri wa miaka 64 aliwahi kusema kwamba ubahili wake ulianzia toka mama yake alipokuwa mtoto. “Mama yangu amekua kwenye mporomoko wa uchumi ndio maana sina meza za gharama kubwa ofisini kwangu,” aliiambia Financial Times.
Bilionea huyu ambaye ametokea kwenye umaskini huwa anafunga chakula kwenda nacho kazini kila siku, na ni mpaka hivi karibuni alipoamua kubadilika, lakini alikuwa kwenye safari zake zote anachanga pesa na kulala chumba kimoja na watu anaosafiri nao.

Azim Premji, anaendesha magari yaliyotumiwa na mara zote huwakumbusha wafanyakazi wake wazime taa wanapozisahau

Kiasi cha utajiri: dola bilioni $15.6 (trilioni 34.9)
Huyu ndiye tajiri namba moja nchini India katika sekta ya teknolojia. Ana umri wa miaka 71 na ana utajiri wa zaidi ya shilingi trilioni 34.9 lakini hili halimzuii kupanda bajaji anapofika uwanja wa ndege kuelekea nyumbani kwake, au kuweka matangazo chuoni akiwataka wafanyakazi wake watumie taratibu karatasi za chuoni (toilet paper)
Bilionea Premji pia anapanda daraja la kawaida kwenye ndege , anaendesha magari yaliyokwishatumiwa, na huwakumbusha wafanyakazi wake wasisahau kuzima taa wanapotoka ofisini ili kupunguza gharama za bili ya umeme wa ofisi.

Judy Faulkner anasema hajawahi kutamani kuishi kifahari

Kiasi cha utajiri: dola bilioni 4.82 (trilioni 10.8)
Mwanamama huyu bilionea mwenye aibu kubwa kwa vyombo vya habari alianzisha kampuni binafsi ya kutoa ya teknolojia inayotengeneza mifumo ya kiteknolojia ya kuhifadhi kumbukumbu za afya na kitabibu — mwaka 1979.
Mafanikio ya kampuni ya mwanamama huyu mwenye umri wa miaka 73 yamemfanya awe bilionea lakini hajawahi kufanya matumizi ya kifahari kama pesa zake zilivyo. Kwa mujibu wa ripoti kadhaa, kwa miaka 15 iliyopita, Faulkner amemiliki magari mawili tu. Pia, yeye na mumewe wameishi kwenye nyumba moja tu iliyopo Madison, Wisconsin, kwa karibia miaka 30 sasa.
Mwezi Mei mwaka 2015 kwenye barua yake ya ahadi ya kutoa nusu ya utajiri alionao, Faulkner aliandika, “Sikuwa hata mara moja kutamani kuwa bilionea ninayeishi maisha ya kifahari na anasa” na akasema kwamba, badala yake, atatumia fedha zake kusaidia watu waweze kupata “chakula, umeme, makazi, huduma za afya na elimu.”

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: NJIA WANAZOTUMIA MABILIONEA KUBANA MATUMIZI ILI WAFANIKIWE ZAIDI
NJIA WANAZOTUMIA MABILIONEA KUBANA MATUMIZI ILI WAFANIKIWE ZAIDI
https://2.bp.blogspot.com/-VRhoN_eTfb0/WX8O5Gb6RNI/AAAAAAAAdM8/TUcqiBvKuxE3wJYVttEuLaBCV7pt3V52QCLcBGAs/s1600/xmaxresdefault-3-750x375.jpg.pagespeed.ic.pinr74j1e6.webp
https://2.bp.blogspot.com/-VRhoN_eTfb0/WX8O5Gb6RNI/AAAAAAAAdM8/TUcqiBvKuxE3wJYVttEuLaBCV7pt3V52QCLcBGAs/s72-c/xmaxresdefault-3-750x375.jpg.pagespeed.ic.pinr74j1e6.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/07/njia-wanazotumia-mabilionea-kubana.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/07/njia-wanazotumia-mabilionea-kubana.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy