OMMY DIMPOZ: SIJAIBA WIMBO WA ‘CHECHE’

Msanii Omari Nyembo a.k.a. Ommy Dimpoz anayetamba na ‘Cheche,’ ameamua kufunguka na kukana tuhuma za kuiba wimbo huo kutoka kwa msanii mwingine anayefanya kazi na Abby Daddy ambaye ni mtayarisha muziki wa BongoFleva. Amekana kuiba wimbo huo kwa kuwa wimbo wenyewe uliandikwa na kufanyiwa kila kitu na msanii Goodluck Gozbert, ‘Lollipop’ na yeye akauchukua kutoka kwake, hivyo hahusiki na mtu mwingine kusema ameibiwa wimbo huo.
Dimpoz alitoa ufafanuzi huo kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha runinga cha EATV baada ya kuwepo kwa maneno kutoka kwa msanii wa Abby Daddy aliyedai kuwa Dimpoz ameiba wimbo huo kutoka kwake. Alisema kuwa yeye hapaswi kuhusishwa hata kidogo kwani alifuata utaratibu wote wa kupata wimbo huo, hivyo, mtayarishaji wa muziki, Abby Daddy pamoja na msanii wake wanapaswa kumalizana na ‘Lollipop’ na si yeye na kwamba ataendelea kuipa promo kazi hiyo kwa kuwa tayari ameshawekeza tayari ikiwa ni pamoja na kuifanyia video.
Akielezea historia ya kuupata wimbo huo, Dimpoz alisema: “Lollipop alinisikilizisha ‘chorus’ hiyo ya (wimbo wa) ‘Cheche’ nikaipenda ila akaniambia wimbo huu haujakamilika. Baada ya hapo aliutengeneza wimbo ule mwanzo – mwisho kwa kuweka sauti zake. Mimi nilichofanya ni kufatisha kisha kile ambacho yeye amefanya. Sijaandika chochote, wala kutunga melody wala chochote kile,” alifafanua Dimpoz na kuongeza:
“Baada ya wimbo kutoka, ambao nilikuwa nao zaidi ya mwaka mmoja, kijana ndio ananiambia kuwa wimbo ni wa kwake. Mimi ikabidi nimuulize Lollipop. Akasema kuwa yeye alikwenda studio ya Abby Daddy kufanya kazi nyingine, baadaye akatengeneza kiitikio hicho na kuingiza sauti lakini Abby Daddy akasema kuwa amependa kiitikio hicho atumie msanii wake sababu yeye Lollipop haimbi nyimbo za hivi. Yeye anaimba nyimbo za dini tu. Ila naomba mumtafute Lollipop mwenyewe aweze kuliongelea zaidi.”
Alisema kuwa hajui kilichotokea kati ya Abby Daddy na Lollipop na hamlaumu yeyote kati yao ila aliomba wasimhusishe kwenye mambo yao. Wamuache aendelee na mambo yake kwa sababu hawezi kurudi nyuma. Dimpoz ameahidi kuachia video ya wimbo huo wiki ijayo.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post