PAMOJA NA KUSHINDA TUZO, MWENDOKASI KUBORESHWA ZAIDI

Ikiwa ni wiki kadhaa toka jiji la Dar es salaam lipewe tuzo ya kimataifa ya ubora wa huduma kupitia mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART) kama inavyojulikana kwa wengi kwa jina la “Mwendokasi,”Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni inayotoa huduma katika mradi huo wa Mwendokasi (U-DART), David Mgwassa amesema kuwa watafanya mambo mazuri zaidi.
“UDART tutaongeza ufanisi katika utoaji wa huduma. Tunawahakikishia wateja wetu kuwa tatizo lolote litakaloripotiwa kwetu litatatuliwa ndani ya dakika 15 tu,” amesema Mgwassa. Pia ameongeza kuwa vigezo vilivyoupa mradi huo tuzo vitazingatiwa na kuboreshwa ili huduma iendelee kukubalika zaidi.
Naye Mtendaji Mkuu wa mradi huo, Ronald Lwakatare amesema kuwa: Heshima hii imetokana na ushirikiano uliopo miongoni mwa wadau wa huduma hizi pamoja na wananchi walioupokea mradi kwa moyo mkunjufu.” Miongoni mwa changamoto ambazo Lwakatare amepania kuziondoa ni uhaba wa kadi za kielektroniki za kusafiria.
Mwanzoni mwa mwezi huu, mradi wa DART ulipewa tuzo ijulikanayo kama “Sustainable Transport Award, (STA)” kwa Kiswahili Tuzo ya Huduma ya Usafiri Endelevu kutokana na ubora wa miundombinu ya mradi huo pamoja na huduma zake katika sherehe za ugawaji wa tuzo hizo zilizofanyika jijini Santiago, Chile.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post