PICHA 5: MBUNGE JULIANA SHONZA ALIVYONUSURIKA KUPIGWA NA WABUNGE WA CHADEMA

Mbunge wa Viti Maalum wa CCM, Juliana Shonza alinusurika kupigwa na wabunge wanane wa CHADEMA kwa kile kinachodaiwa kuwa aliwatukana kwa kuwaita wapumbavu.
Wabunge hao walidai kuwa Shonza waliwaita wapumbavu baada ya kumwambia kuwa, anachofanya bungeni hasa kuwasilisha mapendekezo ya adhabu dhidi ya Wabunge wa CHADEMA, Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda Mjini) ni chuki binafsi ya kuondoka upinzani.
Wabunge hao (bonyeza hapa kuwafahamu kwa majina) wa CHADEMA walitaka kumpiga Shonza walipokuwa wakisubiri kukaguliwa ili kuingia jengo la utawala kwa ajili ya kikao chao cha waandishi wa habari.
Wabunge wanaotuhumiwa kuhusika katika tukio hilo wamehojiwa na Polisi usiku wa kuamkia leo na pia Spika wa Bunge amesema atalifikisha suala hilo katika Kamati ya Maadili ili iweze kulijadili.
Hapa chini ni picha 5 za tukio hilo;

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post