PICHA 5 ZA MAAJABU NGORONGORO, SIMBA ANASWA AKIMNYONYESHA MTOTO WA CHUI

Miongoni mwa picha za matukio machache ambazo utazishuhudia dunia ni pamoja na hii iliyotokea katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro nchini Tanzania ambapo Simba ameonekana akimnyonyesha mtoto wa Chui.
Picha hii ilipigwa na Joop Van Der Linde ambaye alikuwa katika ziara ya kitalii kwenye Ndutu Safari Lodge katika hifadhi hiyo.
Simba huyo anaonekana akiwa amelala chini kwa utulivu kana kwamba anamnyonyesha mwanae wa kumzaa. Hili si jambo la kawaida kuona mnyama wa aina moja akimnyonyesha mtoto wa jamii nyingine.
Simba huyo ambaye aemfungwa kifaa cha kuweza kutambua alipo (GPS) alikuwa na watoto wake watatu waliozaliwa kati ya Juni 27-28.
Kiongozi mmoja anayefanya kazi katika hifadhi hiyo alisema kuwa tukio hilo ni la kipekee sana na hana uhakika kama limewahi kutokea kwa wanyama wakubwa kiasi hicho.
Dr Luke Hunter aliiambia BBC kuwa hajawahi kushuhudia tukio kama hilo kwani mara nyingi Simba huweza kuwachukua watoto wa jamii yake na kuishi nao na si wa jamii nyingine.
Kwa kawaida simba akikuta mtoto wa chui humuua kwani anamuona kama mshindani mwingine katika mfumo mzima wa upataji chakula (food chain), alisema Dr Hunter alipokuwa akielezea tukio hilo la ajabu.
Simba huyo alionekana akimnyonyesha mtoto wa chui wakati watoto wake waliozaliwa wiki mbili zilizopita wakiwa wamejificha.The lioness lies down with her eyes closed as the leopard cub feedsThe leopard cub turns to face the camera between nursingA close-up of the leopard cub suckling as the lioness looks onA shot of the leopard cub crouching with its tale extended

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post