PICHA: OMMY DIMPOZ APATA DILI KAMA LA ALIKIBA

Mwanamuziki Omar Nyembo maarufu kwa jina la sanaa, Ommy Dimpoz amesaini mkataba na lebo ya RockStar4000 ambapo kuanzia sasa kazi zake zitashughulikiwa nao.
Ommy Dimpoz ambaye awali alikuwa chini ya lebo ya Pozi Kwa Pozi (PKP) amesaini dili hilo akiungana na mwamuziki Alikiba ambaye amekuwa akifanyakazi na RockStar kwa muda sasa.
Akiwataarifu mashabiki wake kuhusu uamuzi huo, kupitia ukurasa wake wa Instagram Ommy Dimpoz aliandika kuwa, kwa sasa amesaini mkataba na kampuni kubwa ya muziki barani Afrika, RockStar4000 ambao ndio watakuwa wasimamizi wa kazi zake.
Ommy Dimpoz amewataka mashabiki wake pia kujiunga na RockStarTv ili kuweza kupata nyimbo zake zaidi.
“My fans! Its official, I’ve signed with the biggest music company in Africa #RockStar4000 as my new management team and with the Premiere Pan African Music Entertainment content & News Channel #RockstarTV! Check out and subscribe to get more Ommy Dimpoz exclusives on #RockstarTVon the leading Cable & Satellite Broadcast TV channels, on mobile networks in your country.”


JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post