PICHA: SHABIKI AKAMATWA KWA KUVAMIA UWANJANI NA KUMKUMBATIA ROONEY

Utafanya nini ikitokea yule mtu ambaye mara nyingi huwa unamuangalia kwenye runinga na unatamani kukutana naye akiwa hatua chache kutoka ulipo simama lakini huruhusiwi kumkaribia kutokana na ulinzi aliowekewa?
Kwa shabiki huyu wa Manchester United jibu lilikuwa ni rahisi kabisa, unapita ukikimbia bila kujali nini kitatokea baada ya hapo na ukamkumbatie mtu huyo.
Kijana huyo aliyefahamika kwa jina la Hassan Junior ekamatwa na Polisi baada ya kuvamia uwanjani na kwenda kumkumbatia Wayne Rooney wakati wa mchezo katika ya Gor Mahia ya Kenya na Everton ya Uingereza uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Rooney ambaye amerejea klabuni hapo akitokea Man United alimkumbatia shabiki huyo aliyeshindwa kujizuia na kukaa kitako.
Mchezo huo umemalizika kwa Everton kuibuka na ushindi wa 2-1 ambayo Rooney amefunga goli lake la kwanza katika dakika 34 ya mchezo na ikiwa ni mchezo wake wa kwanza tangu asajiliwe na Everton.
Hapa chini ni video ya goli la Wayne Rooney.
Pitch invader hugs Rooney as team mates look onPitch invader hugs Rooney as team mates look onPitch invader hugs Rooney as team mates look on
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post