PICHA: TUNDU LISSU AENDA MAHAKAMANI NA FULANA YA UKUTA

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu jana alikuwa kivutio baada ya kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akiwa mavelia fulana ya UKUTA huku akionyesha alama ya videole viwili ambayo ni salamu ya CHADEMA.
Tundu Lissu alifika mahakamni hapo na kusomewa shtaka la uchochezi kufuatia kutoa hotuba ya kichochezi dhidi ya Rais Dkt John Pombe Magufuli eneo la Ufipa Kinondoni.
Mbali na kesi hiyo kuzua hisia tofauti miongoni mwa watu mbalimbali, lakini pia fulana hiyo ya Lissu ilizua gumzo kufuatia serikali kuzipiga marufuku fulana hizo zilizodaiwa ni za kichochezi.
UKUTA ni kifupi cha Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania operesheni ambayo ilikuwa imeanzishwa na CHADEMA mwaka jana kwa kile walichodai kuwa ni kupinga kuminywa kwa demokrasia pamoja na haki za binadamu nchini.
Wengi waliohoji ujasiri wa Lissu kuvaa fulana hiyo angali yupo mahakamani, huku yeye mwenyewe akiwauliza wafuasi wa CHADEMA waliokuwa mahakamani hapo, kwanini hawakuvaa kama yeye.
Baada ya kusomewa shtaka hilo Lissu ambaye ni Rais wa TLS alirudishwa rumande na kesi hiyo itaendelea tena Julai 27 mwaka huu.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post