PIGO KWA SIMBA, AISHI MANULA HATIHATI KUTOCHEZA LIGI KUU

Timu ya Simba imeshaanza maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa 2017/18 lakini kuna utata umeibuka kuhusu kipa Aishi Manula ambaye ilidaiwa kuwa Simba wamemsajili akitokea Azam FC.
Taarifa kutoka ndani ya Azam FC zinaeleza kuwa Simba imeshindwa kumtambulisha mchezaji huyo kwa kuwa mkataba wake unatarajiwa kumalizika Agosti 10 wakati dirisha la usajili linatarajiwa kufungwa Agosti 6, mwaka huu.
Ikiwa Simba haitafikia makubaliano na Azam FC kuhusu kuuvunja mkataba wa mchezaji huyo kuna uwezekano mkubwa basi Manula akakosa michezo ya raundi ya kwanza ya msimu huo unafuata.
Hatua hiyo inaweza kutokea kwa kuwa ili Simba ikamilishe usajili wa Manula inatakiwa kupeleka jina lake kwenye orodha ya majina yao ya usajili kwa TFF kabla ya dirisha kufungwa, kwa kuwa mkataba wake utaisha baada ya usajili kufungwa hilo linaweza kuwa kikwazo kikubwa katika kukamilisha mchakato huo.  
Raundi ya kwanza Ligi Kuu Bara msimu ujao inatarajiwa kukamilika Desemba 25, baada ya hapo kutakuwa na dirisha dogo la usajili kisha raundi ya pili itaendelea Desemba 29, mwaka huu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post