POLISI WAAGIZWA KUWAKAMATA WATUMISHI WA HOSPITALI YA RUFAA YA KITETE

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Thea Ntara amemtaka Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kitete kuwakamata mara moja na kuwafikisha Polisi watumishi wawili wa hospitali hiyo wanaotuhumiwa kukutwa na dawa na vifaa tiba katika mikoba yao.
Dkt. Ntara alitoa kauli hiyo mjini Tabora jana baada ya watumishi hao kukamatwa na vifaa hivyo katika mikoba yao kinyume na utaratibu wa hospitali na ambapo ilidaiwa kuwa walipanga kwenda kuviuza kwenye hospitali binafsi.
Dkt Natara alisema kuwa, baada ya watumishi hao kukamatwa na kupekuliwa katika mikoba yao ndipo walikuwa na dawa na vifaa tiba hivyo ambavyo havikutakiwa kutoka nje ya hospitali na havikuwa na maelekezo ya Mganga.
Watumishi waliokamatwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa na vifaa tiba katika mikoba yao ni Petronila Mbipa Bundala ambaye ni Mhudumu na Monica Alexanda Rugeinamu ambaye ni Muuguzi.
Aidha, Katibu Tawala huyo aliwapongeza walinzi katika hospitali hiyo kwa kufanikisha kuwabaini watumishi hao huku akiwataka kuongeza kupekua watu wote wanaokwenda kuona wagonjwa kwa sababu yawezekana watumishi wengine ambao sio waadilifu wakatumia nafasi hiyo kutorosha dawa na vifaa tiba na hivyo kupelekea upungufu kwenye hospitali.
Alimwagiza Mganga Mfawaidhi wa Hospitali hiyo kuhakikisha watuhumiwa hao wanakamatwa mara moja na kufikishwa Polisi wakati hatua nyingine za kiutumishi zinaendelea.
Vifaa tiba vinavyodaiwa kukamatwa ni pamoja na Cannula, Surgical gloves, Syringesa, Urinal bag, IV giving set, Blood giving set, Brainded silk number, water injection, powder, soap, examination grolve, gentamyacin injection ampule, ascorbic acid.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post