POLISI WATOA MAJINA NA PICHA ZA WAUAJI WA KIBITI WANAOTAFUTWA

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Eng. Hamad Yussuf Masauni ametangaza kuwa, Jeshi la Polisi linawaska watuhumiwa 16 wa mauaji ambayo yamekuwa yakiendelea kufanyika katika maeneo ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani kwa muda mrefu sasa.
Masauni amesema jeshi jilo litatumia nguvu zote inazoweza kuweza kukomesha mauaji hayo ili wakazi wa eneo hilo waweze kuishi kwa amani na kurudi kwenye maisha yao ya kila siku.
Akitaja baadhi ya majina ya watuhumiwa hao wanaotafutwa alisema ni pamoja na Hassan Haruna Kyakalewa Shujaa, kutoka Ikwiriri mwenye umri kati ya miaka 25-35. Mwingine ni Omari Abdallah Matimbwa.
Wengine  wanaosakwa na jeshi hilo ni, Anafi Rashid Kapera kutoka Kibiti mwenye miaka kati ya 25-30 mrefu wa wastani, mwenye uso wa mviringo na wa mwisho ni, Faraji Ismail Nangalava kutoka Kibiti mwenye kati ya miaka 25-35.
Masauni aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema Jeshi la Polisi lina picha za watuhumiwa wote wanaotafutwa.
Aidha Jeshi la Polisi lilisema kuwa, zawadi nono itatolewa kwa watakaofanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post