RAIS KIKWETE AKOSOA WANAOZUIA WATU KWENDA KUTIBIWA NJE

Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete jana aliibuka na kutolea utetezi kufuatia Benki ya Dunia (WB) kukosoa serikali za nchi za Afrika Mashariki namna zinavyoshughulikia maendeleo ya sekta ya afya, na jinsi viongozi walivyoshindwa kuboresha huduma hiyo muhimu kwa jamii, huku wao wakisafiri kwenda nje kutibiwa.
Akizungumza katika ufunguzi wa watoa huduma za afya, wamiliki wa vituo vya afya na wataalamu wa afya kutoka nchi za Afrika Mashariki na nje ya Afrika, Rais Kikwete alisema kuwa, kusimama kwenye majukwaa na kusema kuwa, watu kwenda kutibiwa nje ya nchi ni kupoteza fedha, jambo hilo si sahihi.
Alisema, serikali za Afrika Mashariki zimekuwa zikijitahidi sana kuhakikisha zinaboresha sekta za afya, lakini akatahadharisha kwamba, maendeleo ya kiwango cha juu kama nchi zilizoendelea hayawezi kupatikana kwa usiku mmoja.
Akieleza sababu kubwa inayopelekea watu kwenda kutibiwa nje ya nchi, Rais Kikwete alisema ni kutokana na upungufu wa wataalamu katika nchi hizo. Akitolea mfano Tanzania ambapo kuna wataalamu watatu wa upasuaji wa mishipa ya fahamu ambapo kwa kawaida hawawezi kuwahudumia wananchi ambao ni milioni 50.
Rais Kikwete aliisihi Benki ya Duania (WB) kutumia suala hilo kama changamoto kwa kuziwezesha nchi za Afrika Mashariki kuboresha sekta ya afya badala ya kutoa lawama kwamba serikali hazifanyi jitihada jambo ambalo si sahihi. Wananchi wanalalamika, sasa na wewe (mwakiliashi wa WB) hautakiwi kuwa katika nafasi ya kulalamika bali kuhakikisha fedha za kuboresha sekta ya afya zinaletwa, alisema Rais Kikwete.
Akizungumza kabla ya Rais Kikwete, mwakilishi wa WB, Khama Rogo alionyesha kushangazwa na wananchi wa nchi hizo kupoteza maisha kutokana na magonjwa kama vile, malaria, kutapika, kuharisha huku viongozi wa nchi hizo wakienda kutibiwa nje ya nchi.
Rogo alisema mara nyingi huwa anasikia viongozi wa Afrika wamekwenda kupatiwa matibabu nje ya nchi jambo ambalo yeye linamkera kwani anaona badala ya wao kuimarisha miundombinu ya ndani wanapoteza fedha nyingi kwenda kutibiwa nje ya nchi. Katika hali ya masikitiko, alisema, mara nyingi anaposikia suala la afya kutoka nchi za Afrika, ni mtu amefariki.
Mkutano huo uliohudhuriwa na nchi 12 pia ulituma ujumbe wa wahudumu katika sekta ya afya, kutoa huduma sahihi na kwa wakati ili kuweza kupunguza vifo vinavyoepukika.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post