RAIS MAGUFULI AMUONYA LOWASSA

Rais Dkt John Pombe Magufuli amewataka wanasiasa wanaoshindwa ku-control (kuitawala) midomo yao na wanzaa kuzungumza mambo ya ajabu wasiyoyajua, ni heri wakanyamaza wakati serikali inafanya kazi zake.
Rais Magufuli amesema kuwa serikali inashughulikia mambo mengi na kwamba kuna watu wengi zaidi ya 35 wameuawa mkoani Pwani lakini hakuna mtu hajalaani ila kwa kutaka isfa za kisiasa anatoka na kuanga kusema hawa wameshikiliwa muda mrefu. Mtu huyo anasahau kuwa hata wahalifu wa Marekani walikaa Guantanamo kwa miaka mingi.
Dkt Magufuli amerusha madongo hayo leo asubuhi alipokuwa katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya upanuzi na ujenzi wa bandari ya Dar es Salaam ambapo alisema, upanuzi huo ukikamilika utasaidia meli nyingi kuja lakini pia utaondoka ama kupunguza kwa kiasi kikubwa ucheleweshaji uliopo sasa bandarini.
Licha ya kuwa Rais Magufuli hakumtaja jina kiongozi huyo aliyekuwa akimsema, ni dhahiri kuwa alikuwa akomuongelea Lowassa ambaye siku za karibuni amekuwa kwenye mvutano na Polisi kufuatia kauli yake aliyoitoa kuhusu Masheikh wa Uamsho kuwa wameshikiliwa na serikali kwa muda mrefu.
Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, aliwataka waumini wa dini ya Kiislamu kutokuwa wa baridi sana na badala yake watumie lugha nyingine tofauti na maneno ambayo serikali itaelewa. Zaidi ya hapo alisema serikali iwafikishe mahakamani ili kesi yao ya ugaidi inayowakabili iweze kutolewa maamuzi.
Wakati akigombea Lowassa aliahidi kuwa kama angeshinda kiti cha urais angewaachia huru viongozi hao wa dini kwani anaamini kuwa hawana makosa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Magufuli alisema viongozi hao wanawafanya waamini kuwa huenda na wao ni wahusika katika matukio hayo, huku akiwaonya kuwa wasiombe serikali ifike huko kwa sababu wataumia.
“Juzi mtu amekamatwa na uniform (sare) 5,000 za JWTZ na inaonekana anahusika na hao walioko ndani, halafu unasema wamekaa muda mrefu, au na wewe ni miongoni mwa waliogiza hizo uniform (sare) za jeshi,” alisema Rais Magufuli.
Katika masuala mengine, Rais Dkt Magufuli ameshangazwa na uwepo wa vichwa 13 vya treni katika bandari ya Dar es Salaam ambavyo mmiliki wake hajulikani. Sasa nyie mna vichwa vya treni hapa na mmiliki wake hajulikani, mliachaje meli ikishusha mzigo bila kuuliza? alihoji Rais.
Kuna vichwa 13 vya treni vimeshushwa hapa lakini havijulikani ni vya nani, tena inasemekana ni vibovu na TRL wamesema hawajaagiza na wala hawajasaini mkataba wowote. Hamkuuliza vya nani baada ya meli kuondoka ndio mnauliza, siku nyingine si watakuja kushusha hata na vifaru au makontena ya sumu. Sijui haya mavichwa mtafayanyia nini, lakini hili ni lazima lisemwe ili Watanzania wafahamu. Tutangulize uzalendo wa nchi yetu “ alizungumza Rais akionesha kushangazwa na tukio hilo.
Hapa chini ni dondoo za mambo mengine aliyoyazungumzia Rais wakati wa hafla hiyo;
1. “Inaonekana kina mama wanaosimamia mashirika ya maendeleo wanafanya kazi nzuri, hata huu mradi ambao umegharimu zaidi ya bilion 900 umewezeshwa na wao.”
2. “Ufanisi na utendaji mzuri wa reli ya standard gauge utategemea ufanisi wa bandari hii, hivyo mtaona ni jinsi gani ni muhinu. Upanuzi huu utaongeza shehena ya mizigo na hivyo kuwezesha serikali kukusanya mapato.”
3. “Mradi huu wa upanuzi na ujenzi wa bandari unatarajiwa kukamilika kwa miezi 36 kama mkataba unavyosema, lakini,nataka miezi 30 iwe imekamilika lakini ikiwezekana hata miezi 28, fedha zipo sasa wakae miezi 36 hapa wanafanya nini.”     
4. “Bandari ilitakiwa iwe imepanuliwa zamani, wafanyabiashara walikuwa wanalamimika bila kusema sababu, tulikuwa na eneo ambalo halitoshi labda ulete mitumbwi na viboti hivi. Tulikuwa tunasema tuna bandari lakini kumbe upande mmoja ni bandari na upande mwingine ni mwalo.”                   
5. “Ikishakamilika bandari hii itakuwa ni ya mfano kwa sababu zitakuwa meli nyingi zinakuja kwa wakati mmoja, kutakuwa hakuna ucheleweshaji labda kama TPA wacheleweshe kwa makusudi na hao watakaochelewesha ndio tutalala nao vizuri.”
6. “Pakiwa na facility nzuri hapa tutakuwa tunapromote uchumi wa nchi zingine. Bahati nzuri sisi ni wanachama wa SADC na EAC, hivyo watu kama milioni 500 watanufaika na bandari hii.”
7. “Serikali ya wamu ya tano imedhamiria kuboresha miundombinu ya usafiri na kudhihirisha hilo, tunaendelea na upanuzi wa bandari mbalimbali, viwanja vya ndege na barabari.”
8. “Bandari mmeanza vizuri lakini nataka kwenye hizi ICDs, hizi ziliwekwa kwa ajili mizigo ikijaa hapa ndio ipelekwe kule lakini sasa hivi inapelekwa hata kabla haijajaa na kuna kamchezo fulani. Mizigo inasemwa ni transit lakini inauzwa humu humu, kuna kampuni fulani inafanya huo mchezo wa kukwepa kodi fuatilieni hilo.” 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post