RAIS MAGUFULI APIGILIA MSUMARI UAMUZI WAKE KUHUSU WANAFUNZI WENYE MIMBA

SHARE:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 4 Julai, 2017 amehitimisha ziara yake ya kikazi ya Sik...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 4 Julai, 2017 amehitimisha ziara yake ya kikazi ya Siku Mbili Mkoani Mwanza kwa kuzindua  mradi wa  Uboreshaji wa huduma ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema.
Mradi huo wa maji umetekelezwa chini ya mpango wa maji wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa gharama ya shilingi bilioni 22.4. Mradi wa Maji Safi mjini Sengerema ulioanza tangu mwaka 2011 unatarajiwa kuwahudumia wakazi 138,000 ifikapo mwaka 2030.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi huo, Mhe. Rais Dkt. Magufuli amesema kukamilika kwa mradi huo kutamaliza tatizo la maji la muda mrefu kwa wakazi wa Sengerema na maeneo ya jirani.
Mhe. Rais Dkt. Magufuli amewataka wananchi wanaozunguka mradi huo kuutunza na kuhakikisha hawaharibu vyanzo vya maji katika eneo hilo la ziwa Victoria ikiwa ni pamoja na kuacha uvuvi haramu ambao umekuwa na madhara makubwa kwa wananchi.
Aidha, ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Mwanza na Vyombo vya Dola kuchukua hatua kali dhidi ya watu wanaochafua vyanzo vya maji katika eneo la Ziwa Victoria.
Katika hafla hiyo ya Uzinduzi wa mradi wa maji  Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA Hamisi Hussein Maarufu TABASAM, ameamua kuachana na chama chake na kujiunga na CCM.
Mhe. Rais Dkt. Magufuli ameendelea kusisitiza msimamo wa Serikali kuwa hakuna mwanafunzi atakayepata ujauzito ataruhusiwa kuendelea na masomo na ameyataka Mashrika yasiyo ya Kiserikali ambayo yamekuwa yakipinga uamuzi huo kufungua Shule zao wenyewe ambazo zitawasomesha wanafunzi wanaopata ujauzito.
”Haiwezekani Serikali itoe pesa kuwasomesha wanafunzi halafu wapate mimba waendelee na masomo hilo haiwezekani, hizo NGOs zinazotetea hali hiyo zikitaka zijenge shule kwa ajili ya kuwasomesha wanafunzi watakaopata ujauzito”amesema Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli amezungumzia uamuzi wa Serikali kupeleka Miswada Mitatu ya dharura Bungeni kuwa unatokana na umuhimu wa hilo katika kutetea maslahi mapana ya nchi na kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi.
Mhe. Rais Magufuli amewaonya wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi wa Chama hicho kutojihusisha na rushwa kwa vile rushwa ni adui wa haki, hivyo, atakayebainika kutumia rushwa atapoteza sifa ya kuwa Mgombea.
Akizungunzia ujenzi wa barabara ya kutoka Kamanga hadi Sengerama kwa kiwango cha lami, Mhe. Rais Dkt. Magufuli amesema kwa sasa  Serikali imeshampata mkandarasi kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu ili barabara hiyo ianze kujengwa katika kutimiza ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Rais Magufuli pia amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchni kufafanua kwa wananchi na kusimamia uamuzi wa Serikali wa kufuta tozo zaidi ya 80 katika mazazo ya Kilimo, tozo 7 za Mifugo na tozo 5 za Uvuvi ambao lengo lake ni kuwaondolea kero wananchi.
Aidha, amesema Serikali inafanya uchambuzi ili kubaini wale wote waliotoa pembejeo hewa na atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini kusitisha utoaji wa leseni mpya za uchimbaji na halikadhalika leseni ambazo zimeisha muda wake. Ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Geita ambao walizuia msafara wake katika maeneo mbalimbali wakati akiwa njiani kuelekea Chato.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Sengerema,Mwanza
04 Julai 2017.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: RAIS MAGUFULI APIGILIA MSUMARI UAMUZI WAKE KUHUSU WANAFUNZI WENYE MIMBA
RAIS MAGUFULI APIGILIA MSUMARI UAMUZI WAKE KUHUSU WANAFUNZI WENYE MIMBA
https://3.bp.blogspot.com/-5HSNDIFbStI/WVyHrBwzs5I/AAAAAAAAcq4/2Vz4eYOXbKEIfJMU2u7joRWMyR6tvoZqACLcBGAs/s1600/xKIT1-750x375.jpg.pagespeed.ic_.RxO5ZuDH2U.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-5HSNDIFbStI/WVyHrBwzs5I/AAAAAAAAcq4/2Vz4eYOXbKEIfJMU2u7joRWMyR6tvoZqACLcBGAs/s72-c/xKIT1-750x375.jpg.pagespeed.ic_.RxO5ZuDH2U.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/07/rais-magufuli-apigilia-msumari-uamuzi.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/07/rais-magufuli-apigilia-msumari-uamuzi.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy