RAIS MAGUFULI NA RAIS MKAPA WAKUTANA WILAYANI CHATO

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini William Mkapa jana aliwasili wilayani Chato mkoani Geita ambapo leo Jumatatu ya Julai 10 anatarajiwa kukabidhi nyumba kumi kwa Hospitali ya Wilaya ya Chato zilizojengwa kwa ufadhili wa Mkapa Foundation.
Benjamini Wiliam Mkapa ambaye alikuwa ameambatana na Mkewe Mama Anna Mkapa wamepokelewa na mwenyeji wao ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa sambamba na Mkewe Mama Janeth Magufuli.
Katika Msafara huo pia Rais mstaafu Mkapa ameambatana na Balozi wa Japan hapa nchini, Balozi Masaharn Yoshida ambaye Jumatatu ya julai 10,2017 atakabidhi mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti kwa Chama cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato – AMCOSS
Rais Mstaafu Mh Benjamini William Mkapa anatarajiwa pia kuhudhuria mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na Mwenyeji wake ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli siku ya jumatatu ya Julai 10,2017 mkutano utakaofanyika katika uwanja wa Mazaina ulioko mjini Chato majira ya saa tatu asubuhi kwa saa za Afrika ya Mashariki
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post