ROMA : NIKIKUTANA NA MAGUFULI NATANGAZA MATATIZO YANGU

Msanii wa muziki wa hip hop, Roma Mkatoliki ameweka wazi akipata nafasi ya kukutana ana kwa ana na Rais John Pombe Magufuli, atakachofanya ni kumweleza tu shida zake binafsi ili asaidiwe kutimiza ndoto zake.

Rapa huyo amedai unapokutana na Rais kwa dakika chache ni fursa kubwa hivyo lazima uitumie vizuri kwani ukisema uanze kueleza matatizo ya wananchi unaweza kukosa nafasi ya kueleza mambo yako kutokana na kukosa muda.
“Nikikutana na Rais nitamweleza matatizo yangu, anisaidie matreka na mahitaji yangu mengi binafsi. Ukikutana na Rais hutakiwi kupoteza muda kuanza kumwelezea shida za wananchi, nampiga kizinga tu Mh hapa nilipo sina kitu kabisa,” Roma alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.
Aliongeza,”Mimi wakati nafanya wimbo wa Mr President mwaka 2011 nilieleza ndani ya ule wimbo nikikutana na Rais nitamweleza nini, mule nimeyaeleza mambo mengi sana na nilitumia kama dakika tano kueleza yote hayo. Changamoto kubwa ukikutana na waheshimiwa unapata muda mchache sana wa kuzungumza nao, dakika moja, mbili au tatu na hizo dakika huwezi kumwambia kero za wananchi, dakika tatu unamwambia Mh mimi naomba unisaidie hiki na hiki niendeshe familia yangu,”
Rapa huyo hivi karibuni alifanya show yake ya kwanza katika ukumbi wa Dar Live ikiwa na mwezi mmoja na nusu toka atekwe na watu wasiojulikana na baadaye kuachiwa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post