RUBY AJAZWA KIBENDI

JAZA ujazwe! Habari ya mjini kwa sasa inamhusu sexy lady wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’ kujazwa kibendi na staa mkubwa wa muziki huo, licha ya kwamba mwanadada huyo amekuwa akifanya siri.
Chanzo makini kililieleza Ijumaa Wikienda kuwa, Ruby ana ujauzito ambao umekuwa ukimfanya ajifichefiche huku akimficha aliyemjaza kibendi hicho kwa madai kuwa, jamaa aliyempachika kibendi amezaa na wanawake tofauti.
Kama ilivyo desturi yake, Ijumaa Wikienda lilimnyatia Ruby ambaye alikiri kuwa mjamzito, lakini akatia ngumu kumtaja baba kijacho na umri wa mimba yake kwani wakati muafaka haujafika.
“Mimba bado ni changa, siwezi kusema ina miezi mingapi. Kuhusu nimepewa na mwanamuziki mkubwa, siyo kweli ila ipo siku wakati ukifika nitasema ni ya nani,” alisema Ruby
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post