RUNGU LA TCRA LAZIKUMBA KAMPUNI 6 ZA SIMU

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeyatoza faini ya jumla ya shilingi bilioni 10.74 makampuni sita ya simu kwa kosa la kukiuka sheria, kanuni na taratibu na kanuni za usajili wa kadi za simu.
Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema kuwa, kampuni hizo za simu zimekuwa zikikiuka utaratibu wa kusajili kadi za simu lakini pia hawatumii vitambulisho.
Kampuni zilizotozwa faini ni Airtel iliyotozwa Sh1.08 bilioni, Smart Sh1.3 bilioni, Vodacom Sh945 milioni, Zantel Sh105 milioni na Halotel Sh1.6 bilioni.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa, kutokana na kampuni hizo kurudia makosa hayo mara kwa mara wamezitoza faini nyingine ambapo Airtel imetozwa Sh542 milioni, Smart Sh37 milioni, Tigo Sh625 milioni, Zantel Sh52 milioni na Halotel Sh822 milioni.
Kama hiyo haitoshi, kampuni hizo zimetozwa faini ya jumla ya Tsh milioni 500 kila moja kwa kukiuka kanuni za usajili wa kadi za simu na hivyo kuhataraisha usalama wa umma.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post