SAFARI YA AZAM FC KWENDA KWAO NIYONZIMA NI LEO JUMATANO

Kikosi cha Azam FC kimetarajiwa kuondoka asubuhi ya leo Jumatano kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya kupiga kambi kujiandaa na msimu mpya wa 2017/18 unayotarajiwa kuanza Agosti 201.7
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Maganga amesema kuwa ili kuwa fiti kwa mchezo huo, walianza mazoezi mapema tofauti na walivyopanga awali kwa ajili ya safari hiyo ya Rwanda ambako ni nyumbani kwa mchezaji Haruna Niyonzima wa Yanga.

“Tunakwenda Rwanda siyo kwa ajili ya kambi peke yake lakini pia tumepata mwaliko kutoka maalum kutoka kwa klabu ya nchini, Rayon Sports ambayo pia watacheza nayo mechi kadhaa pamoja na kufanya mambo mbalimbali ya kijamii.

“Tumeanza kambi mapema kwa heshima yao, Jumamosi tunatarajiwa kucheza dhidi yao katika sherehe maalum za kukabidhiwa ubingwa wao, ” alisema Maganga.

Baadhi ya wachezaji ambao walianza mazoezi kikosini hapo ni Mwadini Ally, Benedict Haule, Metacha Mnata, Bruce Kangwa, Abbas Kapombe, Ramadhan Mohamed, Abdul Omary, Frank Domayo, Masoud Abdallah, Stanslaus Ladislaus na Yahaya Zaidi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post