SERIKALI YAFUTA RASMI WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI (TMAA)

SHARE:

Bunge  limepitisha sheria mpya ambayo sasa itatambua haki na dhamana ya serikali katika makinikia ambayo itakuwa ni marufuku kuchenjuliwa...

Bunge  limepitisha sheria mpya ambayo sasa itatambua haki na dhamana ya serikali katika makinikia ambayo itakuwa ni marufuku kuchenjuliwa nje ya nchi na serikali itashiriki kwa asilimia kuanzia 16 hadi 50 katika shughuli zote za uchimbaji, uchakataji na uchejuaji madini na ununuzi wa hisa katika kampuni ya uchimbaji madini.
Aidha, Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) umefutwa rasmi na sasa kunaanzishwa Kamisheni ya Madini, na kwamba kuanzia sasa umiliki wa leseni mbalimbali zinazotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Madini, hautahamishwa kabla haujafanyiwa uendelezaji katika kitalu husika.
Akielezea mapendekezo ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2017 katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi alisema asilimia hizo za hisa ni kwa kuangalia thamani ya gharama ambazo serikali inahamia katika vituo vya uwekezaji na kodi aliyopewa mwekezaji.
Profesa Kabudi alisema muswada huo pia unatambua haki na dhamana ya serikali juu ya makinikia na kuweka utaratibu wa kuyahifadhi sehemu maalumu migodini chini ya uangalizi wa serikali.
“Kupitia marekebisho hayo, makinikia yanayotolewa nchini bila kufanyiwa uchunguzi wa kupata thamani halisi kabla ya kuchenjuliwa na uchenjuaji utafanyika nchini. Kuanzia sasa makinikia hayatauzwa nje ya nchi, yatauzwa kwenda kwa wachenjuaji wa ndani ya nchi yakiwa ni bidhaa ambayo itatozwa kodi,” alifafanua.
Alisema pia muswada unaipa serikali haki na dhamana juu ya usimamizi wa bidhaa zote na maliasili, zinazotokana na uchimbaji, uchakataji na uchejuaji wa madini yakiwamo makinikia au kwa jina maarufu mchanga wa dhahabu.
Aidha, alisema muswada umelenga kutambua na kuweka chini ya uangalizi wa serikali maeneo yote ya uchimbaji na madini kwa lengo la kuweka ulinzi na usimamizi madhubuti wa madini kwa lengo la kuweka ulinzi na usimamizi madhubuti wa maeneo ya uchimbaji.
 “Hii itasaidia kuwepo ulinzimahsusi wa maeneo yote ya uchimbaji wa madini, kuwepo kwa utaratibu wa serikali kufanya ukaguzi na udhibiti wa usambazaji wa madini, kuipa serikali uwezo wa kudhibiti na kutambua viwango vya madini yote yanayotolewa kwenye maeneo ya migodi na kupitia vyombo vya ulinzi na usalama vya serikali,”alieleza.
TMAA yazikwa rasmi
Alieleza kuwa kufutwa kwa TMAA kunatokana na majukumu yake, yaliyokuwa yakitekelezwa na wakala huyo kuhamishiwa kwa Kamisheni ya Madini ambayo itaanzishwa.
Akiwasilisha muswada huo, Profesa Kabudi alisema kutokana na kufanyiwa mapitio ya madaraka ya Waziri na Kamishna wa Madini kwa lengo la kuwapunguza baadhi ya majukumu na madaraka yatahamishiwa kwa Kamisheni ya Madini.
Alisema kamisheni inayopendekezwa kuanzishwa itakuwa na jumla ya makamishina tisa, na watu kati yao akiwamo Mwenyekiti watakuwa wa kudumu.
“Watashirikiana na watendaji wakuu kutekeleza majukumu yao ya Kamisheni ya kila siku, makamishna wengine watakuwa wa muda na watakutana katika vikao maalumu vya kamisheni kwa ajili ya kufanya maamuzi ya misingi na kufuatilia utekelezaji wake,” alifafanua na kuongeza kuwa makamishina wa muda watateuliwa kutokana na nafasi zao ambao ni Katibu Mkuu Hazina, Katibu Mkuu Tamisemi, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Mkuu wa Ulinzi na Katibu Mkuu Ardhi.
“Kamisheni inayopendekezwa kuundwa itachukua majukumu sehemu kubwa ya majukumu ya Kamishna wa Madini kwa sasa. Majukumu hayo ni pamoja na kutoa, kuhuisha au pale itakapolazimika kufuta leseni zote zinazotolewa kwa mujibu wa sheria ya madini, kusimamia shughuli za madini ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi maeneo ya migodi.
“Pia majukumu yote yaliyokuwa yakitekelezwa na TMAA yatahamishiwa na kuwekwa chini ya Kamishna. Na kwa msingi huu TMAA inafutwa,” alibainisha.
Umiliki wa leseni 
Kuhusu kutohamisha leseni, alisema hatua hiyo ni katika kuzuia watu kufanya biashara ya udalali wa leseni.
“Katika kuweka masharti yanayokusudia kuzuia watu kufanya biashara ya udalali wa leseni mbalimbali zinazotolewa kwa mujibu wa sheria ya madini, mmiliki wa leseni hataruhusiwa kuhamisha umiliki wa leseni kabla ya uendelezaji katka kitalu husika,” alieleza.
Aliongeza, “baada ya kumalizika kwa muda wake, leseni itahuishwa kwa kipindi kimoja tu, na baada ya hapo umiliki wa kitalu husika utarejeshwa serikalini.”
Chanzo: Mtaakwamtaa

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: SERIKALI YAFUTA RASMI WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI (TMAA)
SERIKALI YAFUTA RASMI WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI (TMAA)
https://2.bp.blogspot.com/-ExL5LYFQdW4/WVzSBVB7ZMI/AAAAAAAAcr0/DOh1JINuMJE71IIZUtbQcJ9qOba8FM2jwCLcBGAs/s1600/testing_tmaa.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-ExL5LYFQdW4/WVzSBVB7ZMI/AAAAAAAAcr0/DOh1JINuMJE71IIZUtbQcJ9qOba8FM2jwCLcBGAs/s72-c/testing_tmaa.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/07/serikali-yafuta-rasmi-wakala-wa-ukaguzi.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/07/serikali-yafuta-rasmi-wakala-wa-ukaguzi.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy