SERIKALI YATANGAZA AJIRA MPYA 10,184

Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imetoa kibali cha ajira 10,184 kwa mamlaka za serikali za mitaa, sekretarieti za mikoa, wakala za serikali, taasisi na mashirika ya umma ili kujaza nafasi zilizoachwa na watumishi wa umma waliokumbwa katika kadhia ya vyeti vya kughushi.
Akizungumza jana katika kikao na watumishi wa umma wa Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki, amesema kuwa, mgawo wa vibali vya ajira umezingatia upungufu uliojitokeza baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma.
Waziri Kairuki alisema utaratibu wa kukamilisha mgao wa nafasi za ajira 4,816 zilizosalia unaendelea ili kutimiza ajira 15,000 zilizoachwa wazi na watumishi mbalimbali.
Katika hali ya kuwatoa wananchi wasiwasi, Waziri Kairuki alisema kuwa mpango wa serikali kutoa ajira mpya upo palepale na kwamba hawa watakaoajiriwa kujaza nafasi hizo wanatakiwa kufika katika vituo vyao vya kazi kuanzia mwezi Agosti.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post