SHULE 10 ZILIZOONGOZA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2017

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA)  limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita leo na wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo  kati ya wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni 27,577 (asilimia 97.21), huku shule za Mkoa wa Pwani ziking’ara miongoni mwa zilizofanya vizuri.
Kwa upande wa wavulana,  waliofaulu ni 42,975 (95.34%) kati ya  46,385 waliofanya mtihani huo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolea inaonyesha kuwa watahiniwa 58,556 (93.72) walipata daraja la kwanza hadi la tatu ambapo kati yao 22, 909 ni wasichana na 35,647 ni wavulana.
Shule 10 zilizofanya vizuri katika mtihani huo na idadi ya wanafunzi kwenye mabano;
  1. Feza Girls’ (67)- Dar es Salaam
  2. Marian Boys (94)- Pwani
  3. Kisimiri (58)- Arusha
  4. Ahmes (40)- Pwani
  5. Marian’s Girls (108)- Pwani
  6. Mzumbe (144)- Morogoro
  7. ST. Mary Mzinde Juu (149)- Tanga
  8. Tabora Boys (129)- Tabora
  9. Feza Boys’ (86)- Dar es Salaam
  10. Kibaha (173)- Pwani
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post