SIMBA WAMFUATA KIUNGO STARS…

Kiungo wa Mbeya City, Raphael Daudi.
ILIBAKI kidogo kiungo anayewindwa na Yanga, Raphael Daudi asainishwe na Simba, baada ya viongozi wa timu hiyo ya Simba kumfuata Mwanza alipokuwa na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, wikiendi iliyopita kwa nia ya kumpa mkataba.
Simba walitaka kuvuruga dili la kiungo huyo wa Mbeya City ambaye amekuwa akimtoa udenda Kocha wa Yanga, George Lwandamina akitaka asajiliwe. Simba walimfuata na mkataba mkononi lakini mwenyewe akawatosa akigoma kusaini huku akiitaka Yanga.
Habari za ndani ambazo Championi Jumatano  limezipata kutoka kwa mmoja wa watu wa Simba, ni kuwa viongozi wa timu hiyo walitaka kuwapiga bao Yanga kwa kumuwahi Raphael, na kumalizana naye wakati akiwa Stars ambayo ilipambana na Rwanda kwenye mechi ya kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Chan ambayo inawahusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani.
“Ilibaki kidogo tu Yanga wamkose Raphael Daud, baada ya wenzao wa Simba kumuwahi hivi karibuni alipokuwa na Stars kwa ajili ya kumalizana naye ambapo viongozi hao walimfuata wakiwa na mkataba kabisa.
“Lakini yeye mwenyewe (Raphael) aliwakatalia kusaini kwa sababu ameshamalizana na Yanga kwa vitu vingi na vilivyobaki kwa sasa ni vidogo huku akitarajiwa kuja Dar muda mfupi akitoka Rwanda kwenye mechi ya marudiano na Rwanda.
“Kama siyo msimamo wa mchezaji huyo basi ungesikia kwamba kiungo huyo ametua Simba kwa ajili ya kuichezea kwa msimu ujao,” kilisema chanzo hicho.
Stori: Said Ally,
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post