STRAIKA WA ZAMANI WA LIVERPOOL AJIUNGA NA AC MILAN

Baada ya Sunderland kushuka daraja, mshambuliaji wa timu hiyo ambaye pia aliwahi kuichezea Liverpool,
Fabio Borini alihusishwa na tetesi za kutaka kujiunga na Lazio na AC Milan na sasa amefanikiwa kurejea kwao Italia.

Mara baada ya klabu hiyo kushuka daraja kutoka katika Ligi Kuu ya England ‘Premier League’, Borini alihusishwa natetesi za kurejea nyumbani kwao Italia ambapo alikuwa akiwaniwa kwa nguvu na timu za AC Milan na Lazio.

Hata hivyo, imebainika kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amekubali kutua San Siro kwa mkopo kipindi cha msimu mzima, huku Milan wakiwa na kipengele kinachowaruhusu kumpa mkataba wa kudumu msimu ujao wa majira ya joto.

Agosti 2015, Sunderland waliilipa Liverpool ada ya paundi milioni 8 lakini Borini alishindwa kufanya vizuri akiwa anacheza kwa mkopo katika kampeni za 2013-14.

Inatimkia Italia akiwa amefunga mabao saba tu katika mechi 50 alizocheza Uingereza kwa miamba hao 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post