TAKUKURU KUWASHTAKI VIGOGO 12 WALIOACHISHWA KAZI NSSF

Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mussa Misalaba amesema kuwa Taasisi hiyo inafanya uchunguzi juu ya wakurugenzi na mameneja 12 waliofukuzwa juzi na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kwamba wakati wowote uchunguzi utakapokamilika watachukuliwa hatua za kisheria.
Vigogo hao waliosimamishwa kazi na Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF mwezi Julai mwaka jana ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha, matumizi mabaya ya ofisi na kutofuata kanuni, sheria na taratibu katika uwekezaji, usimamizi wa miradi, manunuzi ya ardhi na ajira.
“Suala lao lipo mikononi mwetu. Uchunguzi ni mchakato wa muda mrefu, tunalifuatilia swala hili kwa karibu kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa…kwa kawaida jinai (kosa la jinai) haifi hadi mhusika atakapokufa. Sheria inaturuhusu kufanya uchunguzi na kuchukua hatua kulingana na ushahidi uliokusanywa,” amesema Misalaba.
Jumatano ya wiki hii, NSSF ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwamba bodi ya wadhamini ya NSSF iliamua kuwaachisha kazi wafanyakazi hao 12 katika kikao chake cha 72 kilichofanyika Juni 30 mwaka huu.
Kwa mujibu wataarifa hiyo, wafanyakazi hao walisababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 93. Bodi hiyo imesema kuwa inaendelea kufuatilia urejeshwaji wa fedha hizo na imesimamisha utekelezwaji wa miradi yote yenye mikataba mibovu.
Walioachishwa kazi na Bodi ya Wadhamini ya NSSF
 1. Yacob Kidula – aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi
 2. Ludovick Mrosso – aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha
 3. Chiku Matessa – aliyekuwa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala
 4. Sadi Shemliwa – aliyekuwa Mkurugenzi wa Udhibiti, Hadhara na Majanga
 5. Pauline Mtunda – aliyekuwa Mkurugenzi wa Ukaguzi na Mahesabu ya Ndani
 6. Crescetius Magori – aliyekuwa Mkurugenzi wa Uendeshaji
 7. Amina Abdallah – aliyekuwa Meneja Utawala
 8. Abdallah Mseli – aliyekuwa Meneja wa Uwekezaji
 9. Mhandisi John Msemo – aliyekuwa Meneja Miradi
 10. Wakili Chedrick Komba – aliyekuwa Meneja Kiongozi – Mkoa wa Temeke
 11. Mhandisi John Ndazi – aliyekuwa Meneja Miradi
 12. Ramadhani Nasibu – aliyekuwa Meneja Mkuu Usalama
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post