UAMUZI WA MAHAKAMA KUHUSU KESI YA MALINZI NA KATIBU WAKE

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Salestine Mwesigwa wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo na kisha kurudishwa rumande baada ya kunyimwa dhamana.
Viongozi hao wa ngazi ya juu wa TFF wanaokabiliwa na mashtaka 28 wamerudishwa rumande hadi Julai 17 mwaka huu ambapo kesi yao itatajwa tena.
Miongoni mwa mashtaka wanayokabiliwa nayo ni kughushi nyaraka mbalimbali pamoja na kutakatisha fedha kiasi cha Tsh milioni 840. Miongoni mwa nyaraka hizo zilizoghushiwa zilielezwa kuwasaidia viongozi hao kujipatia fedha kwa udanganyifu.
Wakati huo huo, Vigogo wa IPTL, James Rugemalila na mmiliki wa Kampuni ya PAP, Harbinder Seth Singh wamerejeshwa rumande hadi Julia 14 mwaka huu.
Wafanyabiashara hao wamepandishwa kizimbani wakituhumiwa kwa makosa la kuhujumu uchumi wa nchi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post