VIDEO: MAALIM SIEF ATANGAZA MSIMAMO WAKE BAADA YA WABUNGE 8 KUFUKUZWA

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad amesema kuwa ameshangazwa na kuvuliwa ubunge kwa waliokuwa wabunge wanane wa chama hicho na kusema kwamba, njama hizo ni kulenga kuidhoofisha CUF pamoja na UKAWA kwa ujumla.
Maalim Seif aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na mwandishi wa Azam Tv ambapo alisema ameitisha kikao cha Baraza Kuu la Uongozi cha dharura ili kuweza kujadili hali ya chama hicho kwa sasa.
Aidha, Maalim Seif alisema ameshangazwa na uamuzi wa Spika wa Bunge kuwavua ubunge wabunge hao wa viti maalum, akisema kuwa jambo hilo limefanyika kwa haraka sana.
Spika alipokea taarifa ya Lipumba na kusema anashughulikia, lakini siku moja baadae aliwavua ubunge wabunge wetu akisema amejiridhidha kwamba taratibu za chama zimefuatwa. Spika amejiridhisha vipi kwa haraka namna hiyo tena akiwa nje ya nchi? alihoji Maalim Seif.
Kuhusu kikao hicho alichosema kitafanyika kesho (leo), alieleza kwamba maamuzi yatakayotolewa hapo ndiyo watakayoyasimamia kwani hilo ndilo baraza halali na hata Lipumba na Msajili wa Vyama vya Siasa wanalitambua hilo, alisema Seif.
Hapa chini ni mahojiano ya Maalim Seif na Azam Tv wakati wa maandalizi ya kikao hicho jana;

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post