VITU VYA KUFANYA KABLA YA SAA 2 ASUBUHI

SHARE:

Maisha ni mchaka mchaka mpaka mara nyingine unaweza kuona huwezi timiza ndoto zako, na kama umeajiriwa na una familia inayokutegemea, hal...

Maisha ni mchaka mchaka mpaka mara nyingine unaweza kuona huwezi timiza ndoto zako, na kama umeajiriwa na una familia inayokutegemea, hali yaweza kuwa ngumu zaidi.
Kama hutatenga muda kila siku kwa ajili ya kujiendeleza — bila shaka muda wako utatumika ukihudumia watu wengine na kabla hujajua kilichotokea, umri utakuwa umekutupa mkono na uzee kukufika — na kujikuta ukijiuliza muda ulipokimbilia. Kibaya ni kwamba maisha ya watu wengi yamejaa vitu vingi visivyo na umuhimu wowote. Hawana muda wa kujenga maisha yao kabisa.
Wewe ndio mwenye maamuzi.
Inabidi uamue, kwani wewe ndio mwenye maamuzi — kwakuwa usipoamua jinsi ya kuendesha maisha yako, mtu mwingine ataamua jinsi ya kuyaendesha maisha yako. Maamuzi mabaya zaidi ni kutoamua kufanya chochote.
Kwa ratiba hii ya kila asubuhi, maisha yako yatabadilika kwa haraka. Ingawa unaweza kuona ni ratiba ndefu lakini ni rahisi kuifata:

1. Lala kwa saa 7 au zaidi

Usingizi ni muhimu kwa mwili wako kama ilivyo chakula au maji ya kunywa. Pamoja na umuhimu huu mkubwa, mamilioni ya watu hawalali kwa muda unaotakiwa na kujikuta wakipata magonjwa wasiyojua hata chanzo chake.
Faida za kulala kwa muda unaoshauriwa:
Kuongeza uwezo wa kumbukumbu, kuongeza umri wa kuishi, kuongeza ubunifu, kupunguza hatari za kupata msongo wa mawazo, kuongezeka kwa uwezo wa kuzingatia, kuondoa utegemezi wa vilevi na visisimua mwili kama kahawa.

2. Sala au kutafakari

Baada ya kuamka, sala au kipindi cha kutafakari ni muhimu sana ili kuielekeza siku yako kuwaza mambo mazuri. Ukitafakari jambo kwa muda mrefu inasaidia kupata suluhisho lake.
Sala na kutafakari hufanya uwe na shukrani kwa uliyonayo. Watu ni kama sumaku, unaposhukuru kwa yale uliyonayo, unazidi kuvutia mambo mazuri. Kama utaianza kila asubuhi kwa sala na tafakari ya shukrani juu ya maisha yako ya sasa, utavutia mambo mazuri yakutokee. Kwahiyo usikubali kuacha kufanya hivi.

3. Oga maji ya baridi

Kuoga maji ya baridi inasaidia kuimarisha afya ya mwili na akili. Ukifanya hivi mara kwa mara, inaleta mabadiliko ya kudumu kwenye mfumo wa kinga ya mwili, mfumo wa damu na mfumo wa mmeng’enyo wa chakula – jambo linaloboresha maisha yako.
Utafiti uliofanyika mwaka 2007 ulibaini kuwa, kuoga maji ya baridi mara kwa mara inasaidia kuondoa msongo wa mawazo vizuri zaidi kuliko matumizi ya dawa za hospitali. Sababu ni kwamba maji ya baridi yanasisimua mawimbi ya hisia mwilini na kukufanya uwe na furaha.
Pamoja na kuwa na faida, kuna woga wa kuoga maji ya baridi asubuhi. Bila shaka yawezekana ulishawahi kujishawishi usioge kwa siku hiyo kutokana na hali ya hewa ilivyo. Unaweza kujikuta umesimama na kuamua kutooga kabisa kwa sababu hiyo. Lakini ukijimwagia maji ya baridi moja kwa moja, moyo utaanza kwenda mbio kwanza lakini baada ya sekunde kama 20 hivi utakuwa sawa.

4. Mazoezi ya viungo

Ingawa kuna ushahidi wa kutosha juu ya umuhimu wa mazoezi kiafya, tafiti zinaonesha kuwa ni theluthi moja tu ya watu wenye umri kati ya umri wa miaka 25 na 64 wanafanya mazoezi mara kwa mara.
Kama unataka uwe ni miongoni mwa watu wenye afya bora, furaha na kiwango kikubwa cha uzalishaji duniani, jiwekee mazoea ya kufanya mazoezi mara kwa mara. Wengine wakisikia hivi wanaweza kuwaza ugumu wa kwenda gym na kunyanyua vitu vizito, lakini ukweli ni kwamba chochote utakachoamua kufanya ili kuishughulisha mwili wako zaidi ya kiwango cha kawaida cha mazoea yako ya kimaisha ni sawa.
Mazoezi yamethibitishwa kupunguza msongo wa mawazo na wasiwasi. Na pia yana mchango mkubwa sana kukufanya uwe na mafanikio kwa yale unayoyafanya. Kama huujali mwili wako, mambo yako mengi maishani hayatakwenda sawa. Binadamu anakuwa mtimilifu anapojali kila kitu, mwili, roho na akili.

5. Kula walau gramu 30 za protini

Mkufunzi mstaafu wa masuala ya lishe katika chuo kikuu cha Illinois, Profesa Donald Layman, anapendekeza ule walau gramu 30 za protini kwenye kifungua kinywa asubuhi. Pamoja na faida nyingine, protini unazokula asubuhi zinaweza kukusaidia sana kupunguza uzito wa mwili kwa wale wenye uzito mkubwa.
Vyakula vyenye protini nyingi vinafanya ushibe muda mrefu zaidi ya vyakula vingine kwa sababu vinasagwa kwa muda mrefu zaidi. Pia, protini inasaidia kuweka kiwango cha sukari kwenye uwiano mmoja, japo linalosababisha usipate njaa mapema.
Kula protini kwanza kunasaidia kuzuia mwili wako kutamani vyakula vya wanga. Na hivi ndio vyakula vinavyokufanya unenepe na kuongeza uzito kirahisi sana.
Baadhi ya vyakula vitavyokupa protini ya kutosha asubuhi:
  • Kula mayai yasiyopungua mawili (mayai yana kiwango kikubwa cha protini)
  • Au unaweza kunywa mchanganyiko maalumu unaoitwa ‘protein shake.’
  • Na kwa wale wanaoepuka vyakula na bidhaa zitokanazo na maziwa, nyama na mayai, kuna mimea yenye protini pia. Jamii yote ya mikunde, mboga mboga na mazao kama karanga, korosho na mazao yote ya mbegu mbegu yana kiwango kikubwa cha protini.

6. Sikiliza /Soma kitu kitakachokupa muamko wa kufanya jambo

Watu wa ‘kawaida’ wanatafuta cha kuwaburudisha, watu wasio wenye malengo wanatafuta cha kujifunza. Ni kawaida ya watu wenye mafanikio zaidi duniani kusoma angalau kitabu kimoja kwa wiki. Muda wote wanajifunza jambo.
Unaweza pia kirahisi kabisa kutimiza hili kwa kusikiliza kitabu kimoja kwa wiki wakati unafanya shughuli zako nyingine au ukiwa njiani kuelekea kazini, mazoezini au hata shuleni.
Hata ukitumia dakika kati ya 15 na 30 kila asubuhi kusoma au kusikiliza kitu kitakachokufanya upate muamko au kujifunza jambo jipya, itakusaidia kukubadilisha kidogo kidogo na kukufanya uwe bora zaidi ya jana yako. Inakuweka kwenye nafasi ya kufanya kazi vizuri zaidi.
Ukidumu na tabia hii kwa muda mrefu, utajikuta umesoma mamia ya vitabu. Utakuwa na ufahamu japo kidogo kwenye maswala mengi yatakayofanya uione dunia na kufikiria kwa namna tofauti kabisa. Utakuwa na uwezo mkubwa zaidi na urahisi wa kuweza kuhusisha mambo mbalimbali kimaisha.
  1. Fanya japo jambo moja tu katika malengo yako ya muda mrefu
Unapokuwa uananza na kazi nyepesi mwanzo wa siku (ambao ndio muda unaokuwa na nguvu zaidi na akili ikiwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuzingatia), utajikuta katika muda ambao umeshayamaliza mambo haya na unataka kuanza kufanya mambo magumu, akili inakuwa ishachoka, bila shaka na mwili pia. hii itafanya ulisogeze mbele jambo ambalo uliliweka kiporo toka jana kwamba ungeifanya leo.
Kwa sababu hiyo, inabidi ufanye mambo magumu kwanza mapema unapoianza siku. Mambo ya muhimu zaidi yafanywe mwanzo wa siku.
Usipofanya hivi, ni rahisi sana kuimaliza siku ukiwa hujayafanya au kuyamaliza yote na utakuwa umechoka kama uchokavyo siku zote huku ukiwa hujafanya jambo lolote kwa ajili ya kutimiza malengo yako ya muda mrefu. Na hapa utajipa visingizio vingi tu kwamba utayafanya kesho yote uliyotakiwa kufanya leo – lakini tunajua kuwa huwa kesho ikifika, huwa hayafanyiwi kabisa tukijiambia ‘kesho pia ni siku.’
Kaulimbiu yako inakuwa: mambo magumu zaidi nayafanya mwanzo wa sikuFanya mambo uliyotamani kuyafanya siku zote, japo kidogo kidogo kwa kuanzia. Kama ukiwa unapiga hatua moja tu kuelekea kwenye malengo yako ya muda mrefu, utakuja kugundua kwamba malengo hayo hayakuwa mbali kabisa.
Baada ya kufanya haya, haijalishi utafanya nini siku nzima, mambo muhimu kwa siku yako utakuwa umeshayafanya mwanzo. Utakuwa umejiweka kwenye nafasi nzuri ya mafanikio ya malengo yako. Na kwa sababu umefanya haya, utaboresha muonekano wako maishani. Utafanya vizuri zaidi kazini kwako na kwenye mahusiano yako. Utakuwa na furaha zaidi, kujiamini na kuwa na uthubutu zaidi wa kufanya mambo mapya.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: VITU VYA KUFANYA KABLA YA SAA 2 ASUBUHI
VITU VYA KUFANYA KABLA YA SAA 2 ASUBUHI
https://3.bp.blogspot.com/-mLgLAC-hOmk/WViQLhuA-8I/AAAAAAAAclE/9FTaG_QEuI8ZtqnB2JU8XWXvUjhbDO4WwCLcBGAs/s1600/sleep.png
https://3.bp.blogspot.com/-mLgLAC-hOmk/WViQLhuA-8I/AAAAAAAAclE/9FTaG_QEuI8ZtqnB2JU8XWXvUjhbDO4WwCLcBGAs/s72-c/sleep.png
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/07/vitu-vya-kufanya-kabla-ya-saa-2-asubuhi.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/07/vitu-vya-kufanya-kabla-ya-saa-2-asubuhi.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy