WAHUNI WA MWANZA WAMNG’OA KUCHA KAJALA

Muigizaji Kajala Masanja.

STAA wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja hivi karibuni yalimkuta makubwa jijini Mwanza baada kunyofolewa kucha na wahuni alipokuwa kwenye majukumu ya kazi yake anayoifanya kwa sasa ya kampuni ya mchezo wa kubahatisha.
Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Kajala alisema kuwa alikuwa kwenye harakati za kazi yake anayoifanya kwa sasa kwenye kampuni hiyo ambapo alikuwa akigawa tisheti ndipo mashabiki wakaanza kumvuta mkono mpaka kumbandua kucha aliyokuwa amebandika mkononi ambayo iliondoka na ukucha wake na kujikuta akipata jeraha na kumwaga damu nyingi.

Kajala akipozi.
“Yaani mimi nilikuwa sina ili wala lile nagawa matisheti mara wakaanza kunivuta kwa nguvu mpaka wakaitoa kucha yangu, hali hiyo ilinitesa asikwambie mtu jeraha la kucha linauma sana,” alisema Kajala.
Aliongeza kuwa, baada ya kucha yake kubanduka alitoa kilio kikubwa kwani alipata maumivu yaliyosababisha ashindwe kuendelea na majukumu yake.

Kajala Masanja.

“Maumivu niliyopata yalikuwa ni makali mno kiasi ambacho nilishindwa kufanya kazi yangu, nilipata matibabu ambapo kwa sasa naendelea vizuri,” alisema Kajala.
Msanii huyo amewaasa wasichana wenzake kuwa makini na kucha za kubandika kwani zikitoka kwa mtindo huo zinasababisha maumivu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post