WAJAWAZITO WASABABISHA MGANGA MFAWIDHI MLANDIZI KUSIMAMISHWA KAZI

SHARE:

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha  WAZIRI wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amemsimamisha kazi Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya ...

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha 
WAZIRI wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amemsimamisha kazi Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mlandizi, Dk. Mpola Tamambele, kutokana na kushindwa kusimamia maelekezo ya serikali ya kuhakikisha mama mjamzito, mtoto chini ya miaka mitano na mzee wanapata huduma bure.
Kutokana na kutokuwa na mamlaka ya moja kwa moja amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Beda Mmbaga kumsimamisha kazi mganga mfawidhi huyo mara moja wakati uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili zikiendelea .
Amemuelekeza kaimu mkurugenzi huyo pia kuwafuatilia watumishi wa afya kituoni hapo waliohusika kumuagiza mama aliyejifungua Salma Khalifan kwenda kununua vifaa vya kujifungulia vya Tsh 180,000 ili apate huduma.
Aliyasema hayo wakati alipokwenda kutembelea Kituo cha Afya Mlandizi, kabla ya kukabidhiwa kwa magari ya wagonjwa matatu kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo, Hamoud Jumaa.
Waziri huyo alisema yeye hana mamlaka ya moja kwa moja kumsimamisha kazi mganga mfawidhi huyo hivyo anaiachia mamlaka husika isimamie jukumu hilo. Alisema hatokubali kuona watumishi wachache kwenye vituo vya afya, zahanati na hospitali wanachezea maagizo ya serikali.
Alifikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mama aliyejifungua ambae alisema amenunua vifaa vya kufanyiwa operesheni kwa gharama ya sh .180,000. Ummy alisema haiwezekani kuona mama wajawazito wanalipishwa hadi gloves na pamba ili kujifungua wakati serikali yao ilishasema watahudumiwa bure .
Alieleza kwamba, kuanzia sasa waganga wakuu wa wilaya, mikoa na watumishi wa afya wote nchini wahakikishe wanatimiza maelekezo ya serikali kuhudumia akinamama wajawazito na watoto ili kupunguza vifo vya uzazi. Alisema kuwa, watumishi na wauguzi wengi wanajituma na kufanya kazi zao kifanisi ila wapo wachache ambao wanakwamisha juhudi hizo.
“Sitokubali mtumishi anakwenda kinyume na serikali, Rais wetu John Magufuli anasisimamia suala zima la kuboresha huduma za afya, halafu akitokea mtu mmoja mzembe anatuchanganya kwakweli sitoweza kumfumbia macho.”
“Wananchi wamekuwa waoga hata kuingia katika suala la bima ya afya kwa sababu ya mambo kama haya, namsimamisha mganga mfawidhi huyo hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.” alisema Waziri Ummy .
Mbali ya  hayo, Waziri Ummy alibainisha, bajeti ya dawa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imeongezeka ndani ya miaka miwili mfululizo kwenye uongozi wa serikali ya awamu ya tano .
Waziri alisema mwaka 2015/2016 bajeti ya dawa katika halmashauri hiyo ilikuwa mil. 24 na 2017 ilifikia mil.70 na bajeti ya sasa 2017/2018 imefikia sh. mil.101 .
Kwa upande wake mama aliyejifungua kituoni hapo, Salma Khalfani alimweleza Waziri Ummy Mwalimu kwamba aliandikiwa orodha ya dawa za kununua kwenye maduka ya dawa ya nje .
Alieleza, alitakiwa kufanyiwa upasuaji na hivyo kutakiwa kununua dawa na vifaaa tiba, pamba na gloves vya 180,000 akanunue ili aweze kujifungua.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Mmbaga alisema maagizo aliyopewa na waziri ameyapokea na atayafanyia kazi .
Nae Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaaa alisema kumekuwa na malalamiko mengi juu ya wananchi hasa akinamama kulipishwa fedha za dawa na vifaa tiba. Alisema baadhi ya wazee wamekuwa wakishindwa kupewa huduma za afya bila malipo .
Jumaa alimuomba Waziri Ummy Mwalimu kuendelea kushirikiana nae kuwadhibiti watumishi wazembe wanaodidimiza haki za wananchi .

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: WAJAWAZITO WASABABISHA MGANGA MFAWIDHI MLANDIZI KUSIMAMISHWA KAZI
WAJAWAZITO WASABABISHA MGANGA MFAWIDHI MLANDIZI KUSIMAMISHWA KAZI
https://1.bp.blogspot.com/-uYLosnTX7gU/WXg_gVW3w-I/AAAAAAAAdEA/ckavW9k8t8AU20XDHKdDbV9lyUpyIuh6ACLcBGAs/s1600/x6bc472cc-5192-11e7-8a38-d46223a68388-750x375.jpg.pagespeed.ic.CdKxtrbB_T.webp
https://1.bp.blogspot.com/-uYLosnTX7gU/WXg_gVW3w-I/AAAAAAAAdEA/ckavW9k8t8AU20XDHKdDbV9lyUpyIuh6ACLcBGAs/s72-c/x6bc472cc-5192-11e7-8a38-d46223a68388-750x375.jpg.pagespeed.ic.CdKxtrbB_T.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/07/wajawazito-wasababisha-mganga-mfawidhi.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/07/wajawazito-wasababisha-mganga-mfawidhi.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy