WATU 10 WATEKWA WAKIWA MSIKITINI MKOANI LINDI

Jumuiya ya Taasisi ya Kiislamu Tanzania imeitaka polisi nchini kufanya uchunguzi wa haraka waweze kuwapata waumini wao kumi waliotekwa katika mazingira ya kutatanisha wilayani Kilwa mkoani Lindi walipokuwa kwa shughuli ya kuelimisha wananchi juu ya dini ya Kiislamu.
Waumini hao walikuwa katika ziara ya kutoa mafundisho ya dini na walikutwa wamelala kwenye Msikiti wa Ali Mchumo . Watu hao walikuwa wameshatambulishwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania katika Wilaya ya Kilwa katika vyombo vya dola kuhusu uwepo wao katika eneo hilo.
Katibu wa Taasisi hiyo, Sheikh Ponda Issa alisema kuwa, Julai 21 waumini kumi waliokuwa wamelala kwenye Msikiti wa Ali Mchumo walitekwa na watu wasiojulikana na hadi sasa haijajulikana walipo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga amesema kuwa hana maelezo ya kutosha kuhusiana na tukio hilo alipoulizwa na waandishi.
“Hata Mkuu wa Wilaya ya Kilwa ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama alifika katika eneo la tukio lakini bado hatujajua kama kweli tukio hilo lilitokea. Bado tunachunguza,” alisema.
Ponda alisema kuwa, ilipofikia saa 5:30 walitokea watu waliokuwa kwenye magari matano ambao kabla ya kuingia msikitini walipiga risasi kwenye milango na kuta.
“Walikuwa wakitoa Elimu mitaani na jioni wanarudi kulala kwenye Msikiti huo. Majirani walisema watu hao waliingia msikitini na kuanza kuwapiga waumini hao na baadaye waliondoka nao. Tunajiuliza kwa nini hadi sasa vyombo vya dola vimeshindwa kutoa taarifa ya tukio hilo hadharani kama wafanyavyo katika matukio mengine?” alihoji Sheikh Ponda.
Ponda alisema kuwa baada ya watu hao kuondoka na waumini, majirani walikwenda kwenye Msikiti huo na kukuta damu iliyoganda na nguo zilizolowa damu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post