WAZIRI LUKUVI: HATI YA ARDHI SASA NI MWEZI MMOJA TU

Waziri William Lukuvi amewaagiza Maofisa Ardhi kote nchini kuhakikisha kuwa hati za viwanja zinatoka ndani ya mwezi mmoja baada ya muimbaji kukamilisha ujazaji wa fomu zake. Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati akizindua mpango-mkakati wa miaka 20 (Master Plan) wa mji wa Iringa kuwa jiji Juzi.
“Mtu yeyote atakayeona kwamba amelipa kila kitu na amechukua mwezi mmoja (hajapata hati ya kiwanja) simu yangu ipo wazi, muda wote anitumie ujumbe mfupi wa sms (na) nitawashughulikia wahusika,” alisema Lukuvi.
Aidha, Waziri Lukuvi alisema Serikali imedhamiria kumaliza kero zinazotokana na watumishi wa sekta ya ardhi ambao wamekuwa siyo waadilifu kwa kufunga mtambo maalum utakaowezesha utoaji huduma kuwa urahisi.
Waziri Lukuvi amewataka watumishi wa Idara ya Ardhi katika Manispaa ya Iringa pamoja na Halmashauri zote nchini kufanya kazi kwa weledi. Pia amewataka watumishi hao kutatua kero za wananchi badala ya kutumia njia za ujanja ujanja zinazolenga kuwakandamiza wahitaji na kuanzisha migogoro.
Katika hatua nyingine, Waziri huyo amewataka viongozi wanaosimamia mpango huo wa Master Plan ya Iringa kushirikisha mamlaka nyingine zinazotakiwa kutoa huduma za kijamii ili waweze kuanza maandalizi ya kufikisha huduma katika maeneo yanayotakiwa kuendelezwa yaliyoainishwa katika mpango huo.
Mamlaka hizo ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCo) na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Iringa (IRUWASA).
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post