ZANZIBAR: JELA MIAKA 13 KWA KUBAKA ZAIDI YA WATOTO 10!

Mahakama ya Mkoa Mwera imemhukumu kifungo cha miaka 13 Idrisa Ali Idrisa (20) kwa makosa 13 ya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya watoto ikiwamo kubaka.
Akisomewa hukumu hiyo mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Naila Abdulbasit na muendesha mashtaka, Arafa Salum, mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda makosa hayo huko Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja. Aliwatorosha watoto hao ambao wapo chini ya uangalizi wa wazazi wao, akawabaka na kuwakashifu.
Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Novemba 8 mwaka 2016 wakati watoto hao wakiwa wameongozana wakitokea madrasa na walipokuwa njiani aliwaita na kuwapeleka kichakani na kuwafanyia udhalilishaji huo.
“Baada ya kuwachukua watoto hawa kichakani akawatishia mbwa ambaye alikuwa naye na kusema iwapo watapiga kelele atamuamuru mbwa awatafune,” alisema.
Hakimu alisema kuwa watoto hao wote ni chini ya miaka 10 na watoto wanne kati ya hao ni ndugu wa familia moja. Alisema ushahidi uliotolewa na mashahidi 15 wakiwamo watoto hao umemtia hatiani mtuhumiwa huyo na kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 13 na kulipa fidia ya shilingi milioni 3.
HT @ HABARI LEO
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post