ZIGGY: SITAKI KUITWA MSANII WA BONGO MUVI

STAA wa filamu nchini  aliyewahi kung’aa kwenye filamu kama Wake Up, Kalambati Lobo, Handsome Fake na Maziko Saa 6, Sogurd Gurdson almaarufu kwa jina la Ziggy,  amesema anaomba atambulike kama msanii wa filamu Tanzania na si msanii anayeunda Bongo Muvi, kwa sababu Bongo Muvi ni kikundi cha baadhi ya wasanii wenye  umaarufu.
“Mimi ni msanii wa filamu Tanzania,  popote nitakapoenda nitajitambulisha hivyo na itakuwa rahisi mtu kunielewa, ila Bongo Muvi ni kikundi cha wasanii wenye umaarufu wao kwa hiyo sitaki kuitwa msanii wa Bongo Muvi,” amesema hivi karibuni.
Ziggy anatarajia kung’aa tena kwenye tamthiliya ya Michakato itakayoanza rasmi  Agosti 7 mwaka huu kupitia kituo cha runinga cha Clouds TV.
NA ISRI MOHAMED/GPL
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post