AGGREY MORIS NA SURE BOY KUENDELEA KUITUMIKIA AZAM MPAKA 2019

NYOTA wawili wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC ambao ni nahodha msaidizi Aggrey Morris Ambrosse pamoja na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ wameongeza Mkataba wa mwaka mmoja kwa kila Mchezaji kuendelea kuitumikia timu hiyo.
Awali mikataba ya Wachezaji hao ilitarajiwa kuisha mwishoni mwa msimu huu, hivyo kwa kuongeza mikataba mipya, itawafanya wachezaji hao kusalia ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2019.
Sure Boy ameisaidia Klabu hiyo kupanda daraja kucheza Ligi kuu Tanzania Bara mwaka 2008 huku Moris akijiunga na mabingwa hao mwaka 2009 akitokea timu ya Mafunzo ya Visiwani Zanzibar.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post