AJABU: UTAFITI WABAINI KUWA MIMEA HUJUA KWAMBA INALIWA

Wale wanaokula mboga za majani tu mna habari mbaya: Utafiti wa hivi karibuni umeonesha kuwa mimea huwa inatambua kwamba inaliwa. Na huwa haipendi kufanyiwa kitendo hicho.
Uthibitisho kwamba mimea ina ufahamu si habari mpya kabisa, lakini kwa mujibu wa “Modern Farmer”, utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Chuo Kikuu cha Missouri unaonesha kwamba mimea huwa inapata hisia ikiwa inaliwa na huwa inatuma taarifa kwenye majani yote (ikiwemo kutoa kemikali yenye sumu) na kuufanya mmea ujilinde kujaribu kuzuia usifanyiwe kitendo hicho.
Mmea wa Arabidopsis uliofanyiwa utafiti huu wa kisayansi
Utafiti huo umefanywa kwenye mmea unaojulikana kitaalamu kama Arabidopsis, ambao uhashabihiana sana na mimea aina ya brokoli, kale, mharadali (mustard), na mimea ya aina hiyo iliyopo kwenye familia ya “brassica” (aina ya mboga za majani zilizopo kwenye kundi la kabichi ambalo maua yake huliwa) ambayo hutumika mara nyingi kwenye tafiti za kisayansi. Hutumiwa kwenye tafiti kwa sababu ulikuwa ni mmea wa kwanza ambao seli zake zilifanyiwa utafiti wa kisayansi, hivyo, wanasayansi wamekuwa wakipenda kuutumia hata kwenye tafiti nyingine kwakuwa matokeo yake ni ya kuaminika zaidi.
Tukirudi kwenye mada yetu iwapo mimea ina uwezo wa kujua inapoliwa, watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Missouri walianza kwa kurekodi sauti inayotokana na mdudu (kiwavi) anapokula majanai ya mmea huo, kujaribu kuhakiki dhana waliyokuwa nayo kama mmea unaweza kusikia au kuhisi majani yake yakiwa yanatafunwa na mdudu huyo na unachukua hatua gani baada ya kujua kuwa unaliwa. Pili kujua kama utarudia kufanya kitendo cha aina hiyo hata kama utasikia sauti nyingine tofauti na ile inayotokea wakati majani yake yanatafunwa.
Watafiti hao walifanya utafiti wao kwa makini kwa kuja na sauti nyingine zilizofana na zile zinazoletwa kiasili kama sauti ya upepo ambayo mimea yote hukumbana nayo.
Matokeo?
Kwa mujibu wa utafiti huo wa “Modern Farmer,” mmea huo unatoa aina ya mafuta yenye kiasi kidogo cha sumu yanapoliwa na sumu hiyo husambazwa kwenye majani yote ili kufukuza wadudu wanaokula majani yake. Utafiti huo ulithibitisha pia kuwa mmea huo unaposikia sauti ya kiwavi akitafuna majani yake, huwa unaachia kiasi kikubwa zaidi cha sumu hii. Lakini mmea huo haukufanya lolote inapoguswa na, au inaposikia sauti nyingine tofauti na ile ya kuliwa.
“Utafiti wa awali ulilenga kuchunguza inachokifanya mimea ikisikia sauti zilizo katika mpangilio maalum kama ala za muziki,” amesema Heidi Appel, Mkuu wa Idara ya Tafiti za Kisayansi kwenye mimea wa Chuo Kikuu cha Missouri.
“Lakini huu wa sasa umekuwa ni mfano wa kwanza unaoonesha hatua za kujihami zinazochukuliwa na mimea inaposikia sauti inayotokana kutafunwa kwa majani yake na mmoja wa wadudu aliye kwenye mzunguko mmoja wa kiikolojia. Tuligundua kwamba sauti zinazotokana na kutafunwa kwa majani huwa zinapeleka taarifa kwamba kuna mabadiliko ya mfumo wa seli unaendelea kufanyika kutokana na majani yake kuliwa, jambo linalofanya mmea huo utoe kemikali nyingi zenye sumu ili kujilinda kwa kufukuza kiwavi anayekula majani yake,” alimalizia Heidi Appel.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post