ALIYEKUWA DAKTARI WA RAIS KIKWETE AMTETEA MANJI KESI YA DAWA ZA KULEVYA

Daktari, Mohammed Janabi (51) kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu namna walivyouchunguza moyo wa mfanyabiashara Yusuf Manji alipopelekwa hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.
Prof. Janabi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI alisema kuwa, alichunguza moyo wa Manji ambaye pia ni Diwani wa Mbagala kwa tiketi ya CCM ili kuweza kutambua kama vyuma vilivyopo kwenye moyo wake kama vimeziba au la ambapo walibaini kwamba havijaziba.
Janabi ambaye amewahi kuhudumu pia kama Daktari wa Rais wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete aliyasema hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakati akiongozwa na wakili Hajra Mungula kutoa ushahidi mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha.
Akijibu swali la wakili kuhusu athari za kutumia dawa za kulevya aina ya heroine na kuvuta sigara kwa wagonjwa wa moyo, Prof. Janabi alisema kwamba, matumizi ya vitu hivyo hupelekea vyuma kwenye moyo wa mgonjwa kuziba na kufanyiwa upasuaji wa juu zaidi. Lakini daktari huyo alisema kwa Manji nyuma havikuwa vimeziba.
Daktari huyo wa moyo alikuwa akitoa ushahidi wa upande wa utetezi katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Manji.
Daktari huyo aliiambia mahakama kuwa dawa za Benzodiazepines zinazodaiwa kukutwa kwenye mkojo wa Manji na Mkemia Mkuu wa serikali hutumiwa kutuliza maumivu makali na kusaidia wasioweza kupata usingizi ambayo pia ni matatizo yanayowakumba sana watu wenye ugonjwa wa moyo.
Aidha alisema katika matatizo hayo, Manji alikuwa na dawa zake binafsi alizokuwa akitumia ambazo hajui alipewa wapi.
Agosti 25 mwaka huu, mahakama ilimkuta Manji na kesi ya kujibu kuhusu matumizi ya dawa za kulevya ambapo anatarajia kuwaita mashahidi 15 kumtetea.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post