ASKOFU GWAJIMA AONYESHA NDEGE YA KIFAHARI ATAKAYOINUNUA

Wakati kumbukumbu za Gwajima kutangaza kuwa atanunua treni yake na hata Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) kusema kuwa anaweza kufanya hivyo zikiwa hazijawatoka watu wengi kwenye akili, ameibuka tena na kusema kuwa atanunua ndege binafsi (Private Jet) kwa ajili ya kutolea huduma zake.
Gwajima ambaye yupo nje ya nchi kwa muda mrefu sasa amechapisha picha katika ukurasa wake wa Instagram akiwa amesimama mbele ya ndege hiyo na kuandika kwa kiingereza akimaanisha kuwa, karibuni ataileta ndege hiyo Tanzania kwa ajili ya kuendeleza ufalme wa Mungu. Ni wakati wa ufufuo na uzima duniani.
“I will soon bring this Jet to Tanzania for purpose of advancing the Kingdom of God! Its the hour of Life and Resurrection in the World!.”
Askofu Gwajima ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima aliondoka nchini mwezi Juni mwaka huu ambapo amekuwa akifanya ibada katika nchi za Ujerumani Japan na sasa yupo nchini Marekani.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post