AUGUSTINO MREMA ASIMULIA ALIVYOPONA SARATANI

Mwenyekiti wa Bodi ya Parole ya Taifa, Augustino Lyatonga Mrema amemshukuru Rais Dkt Magufuli kwa kumsaidia kwenda nchini India kupatiwa matibabu na kufanikiwa kupona ugonjwa wa saratani uliokuwa ukimsumbua kwa muda.
Mrema ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha TLP Taifa, tangu kuteuliwa kwake na Rais kuiongoza bodi hiyo ya misamaha kwa wafungwa amekuwa hayupo katika afya nzuri.
Wakati akitoa shukrani hiyo, Mrema alisema kwamba kwa sasa ataweza kufanya kazi vizuri kwa kuwa amepona ugonjwa uliokuwa unamsumbua na hivyo kushindwa kuwatumikia wananchi vizuri.
Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama Mkombozi ya Dar es Salaam, Cathbert Magaga ambapo ndipo Mrema alipotolea shukrani hiyo, aliwasihi waumini wengine kuiga mfano huo wa kutoa shukrani pale wanapofanikiwa katika mambo yao.
Mrema alisema mbele ya waumini hao kuwa amefarijika sana kwa ushirikiano na  masaada alioupata kutoka kwa waumini wenzake na viongozi wa serikali.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post