BANGI YAKAMATWA KWENYE MAGUNIA YA MBOGA BANDARINI

Kila uchao, binadamu hujaribu kutafuta mbinu mpya za kupambana na mazingira anayokumbana nayo. Vivyo hivyo kwa wafanyabiashara haramu ya dawa za kulevya.
Baada ya vyombo vya usalama kuziba mianya ya usafirishwaji wa dawa za kulevya kwa kiwango kikubwa ndani na nje ya nchi, sasa wafanyabiashara hao wamebaini mbinu nyingine mpya ya kusafirisha dawa hizo pasipo kutiliwa shaka wala kubainika.
Haya yametokea juzi baada ya maafisa wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kukamata kilo 80 za bangi iliyokuwa imefichwa ndani ya magunia ya kabichi na vitunguu muda mfupi kabla ya kusafirishwa kuelekea Zanzibar.
DCEA imethibitisha kuwa kiasi hicho cha bangi kilisafirishwa kutokea mkoani Morogoro na kushushwa katika soko la Kisutu wakati zoezi la kuificha ili isibainike likiendelea.
Baada ya wahusika kujiridhisha kuwa wameificha vyema bangi hiyo waliipakia katika mkokoteni mmojawapo sokoni hapo na kuipeleka bandarini. Wakati huo maafisa wa DCEA walikuwa wakifuatilia kwa ukaribu kabisa zoezi hilo hatua kwa hatua.
Mzigo ulipofikishwa bandarini katika feri ya kampuni ya Azam, maafisa wa DCEA waliuacha upitishwe kwenye mashine za ukaguzi na waliukamata mara tu uliporuhusiwa kuondoka.
Maafisa hao walipoupekua mzigo huo uliokuwa na mboga walikuta kiasi kikubwa cha bangi kikiwa kimepangwa kwa uangalifu ili kuzuia kubainika.
“Tuliutilia mashaka na tulianza kuwa-track (kuwafuatilia) mapema tangu mzigo ulipoanza safari ya kuelekea bandarini na hatimaye tuliukamata na kuuchambua mzigo wote kupata zaidi ya kilo 80 za bangi,” alisema kamishna mpya wa operesheni wa DCEA, Frederick Milanzi.
DCEA inawashikilia watu wanne akiwamo mwanamke mmoja aliyetambuliwa kuwa mmiliki wa mzigo huo na baba yake mzazi. Mamlaka hiyo inawashikilia pia wakala aliyeupitisha mzigo huo na mtu aliyeusindikiza kutoka soko la Kisutu hadi bandarini.
Baba wa mwanamke huyo anaelezwa kustushwa na tukio hilo na amewaeleza wakamataji kuwa mwanaye alimuomba amsaidie tu kusimamia mzigo wake wa mboga pale bandarini wakati akishughulikia namna ya kuusafirisha.
“Tunaendelea na uchunuzi wa kina. Nia yetu sasa ni kupata mtandao wote wa huku Bara na Zanzibar na hatimaye kuufuta kabisa,” alisema kamishna Milanzi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post