BEKI ALALAMIKA AZAM INAMBANIA KUTOSAJILIWA NA YANGA

Beki wa Azam FC, Gadiel Michael ameijia juu klabu yake hiyo kwa kile alichodai klabu hiyo haionyeshi uungwana kwake kwa kuwa tayari amemalizana na Yanga lakini wanambania kuondoka.
Gadiel ambaye amekuwa akifanya vizuri katika miezi ya hivi karibuni hasa alipokuwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, amesema kuwa mkataba wake na Azam FC umebakisha miezi mitano, lakini tayari ameshasaini mkataba wa awali kuichezea Yanga, lakini Azam FC haitaki kuzungumza na Yanga ili aondoke.
Amedai kuwa alichukua maamuzi ya kusaini mkataba wa awali kuichezea Yanga kwa kuwa hakufikia makubaliano ya kimaslahi ya kusaini mkataba mpya Azam FC, hivyo akaona Yanga ndiyo sehemu sahihi kwake.
Anasema kuwa alienda klabuni Azam FC na kuambiwa hayumo kwenye mipango ya kocha na hata chumba ambacho alikuwa akitumia tayari kimeshachukuliwa na mchezaji mwingine, akaongeza kuwa mabosi wa Azam wamemwambia aende akafanye mazoezi na Yanga jambo ambalo hawezi kulifanya kwa kuwa bado ana mkataba na Azam FC.
Akizungumza zaidi Gadiel alisema: “Mimi nimeshaamua kuondoka, wao Azam wanatakiwa kukaa meza moja na Yanga kuzungumza, najua bado ni mchezaji wao lakini kitendo cha kuniondoa mazoezini kinamaanisha siwezi kucheza, sasa itakuwaje wakati mimi nataka kulinda kipaji change.”
Alipotafutwa Meneja wa Azam FC, Abdul Mohamed alisema atafutwe Gadiel Michael mwenyewe azungumze, pia akaomba apewe muda atajibu hoja hiyo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post